ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

Al-Mutaffifin

external-link copy
1 : 83

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ

Ole wao hao wapunjao! info

Wataangamia wanao punja,

التفاسير:

external-link copy
2 : 83

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ

Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. info

Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,

التفاسير:

external-link copy
3 : 83

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ

Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. info

Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!

التفاسير:

external-link copy
4 : 83

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ

Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa . info

Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,

التفاسير:

external-link copy
5 : 83

لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ

Katika Siku iliyo kuu! info

Katika siku ya vitisho vikuu?

التفاسير:

external-link copy
6 : 83

يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? info

Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?

التفاسير:

external-link copy
7 : 83

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ

Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. info

Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.

التفاسير:

external-link copy
8 : 83

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ

Unajua nini Sijjin? info

Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?

التفاسير:

external-link copy
9 : 83

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ

Kitabu kilicho andikwa. info

Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.

التفاسير:

external-link copy
10 : 83

وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ

Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! info

Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.

التفاسير:

external-link copy
11 : 83

ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. info

Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.

التفاسير:

external-link copy
12 : 83

وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ

Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. info

Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.

التفاسير:

external-link copy
13 : 83

إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ

Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! info

Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!

التفاسير:

external-link copy
14 : 83

كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ

Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. info

Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.

التفاسير:

external-link copy
15 : 83

كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. info

Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.

التفاسير:

external-link copy
16 : 83

ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ

Kisha wataingia Motoni! info

Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.

التفاسير:

external-link copy
17 : 83

ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. info

Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!

التفاسير:

external-link copy
18 : 83

كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ

Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. info

Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.

التفاسير:

external-link copy
19 : 83

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ

Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? info

Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?

التفاسير:

external-link copy
20 : 83

كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ

Kitabu kilicho andikwa. info

Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake,

التفاسير:

external-link copy
21 : 83

يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Wanakishuhudia walio karibishwa. info

Wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.

التفاسير:

external-link copy
22 : 83

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. info

Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi,

التفاسير:

external-link copy
23 : 83

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ

Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. info

Juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.

التفاسير:

external-link copy
24 : 83

تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ

Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, info

Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.

التفاسير:

external-link copy
25 : 83

يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ

Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, info

Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa;

التفاسير:

external-link copy
26 : 83

خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ

Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. info

Kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.

التفاسير:

external-link copy
27 : 83

وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ

Na mchanganyiko wake ni Tasniim, info

Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi,

التفاسير:

external-link copy
28 : 83

عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ

Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. info

Nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.

التفاسير:

external-link copy
29 : 83

إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ

Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. info

Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.

التفاسير:

external-link copy
30 : 83

وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ

 Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. info

Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.

التفاسير:

external-link copy
31 : 83

وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ

Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. info

Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.

التفاسير:

external-link copy
32 : 83

وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ

Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. info

Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad.

التفاسير:

external-link copy
33 : 83

وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ

Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. info

Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.

التفاسير:

external-link copy
34 : 83

فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ

Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, info

Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.

التفاسير:

external-link copy
35 : 83

عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ

Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. info

Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.

التفاسير:

external-link copy
36 : 83

هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? info

Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?

التفاسير: