ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

Al-Qiyamah

external-link copy
1 : 75

لَآ أُقۡسِمُ بِيَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Ninaapa kwa Siku ya Kiyama! info

Ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa Siku ya Kiyama, na hiyo ni kweli iliyo thibiti;

التفاسير:

external-link copy
2 : 75

وَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلنَّفۡسِ ٱللَّوَّامَةِ

Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu! info

Na ninaapa na natilia mkazo kiapo hichi kwa nafsi inayo mlaumu mtu kwa dhambi zake na upungufu wake, ya kwamba bila ya shaka yoyote mtafufuliwa baada ya kukusanywa mafupa yenu yaliyo tawanyika.

التفاسير:

external-link copy
3 : 75

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَلَّن نَّجۡمَعَ عِظَامَهُۥ

Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? info

Hivyo mtu anadhani baada ya kuwa Sisi tulimuumba naye hakuwa kitu chochote, tutakuja shindwa kuyakusanya mafupa yake yaliyooza na yakatapanyika?

التفاسير:

external-link copy
4 : 75

بَلَىٰ قَٰدِرِينَ عَلَىٰٓ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُۥ

Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake! info

Hasha! Sisi tuna uweza wa kuviweka sawa hata vifupa vya vidole vyake vilivyo vurugika, wachilia mbali mafupa yake makubwa makubwa ya mwili wake.

التفاسير:

external-link copy
5 : 75

بَلۡ يُرِيدُ ٱلۡإِنسَٰنُ لِيَفۡجُرَ أَمَامَهُۥ

Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake. info

Hivyo mtu anakanya kufufuliwa? Anataka abakie katika uasi wake katika siku zote zilizo mbakilia katika umri wake ulio salia?

التفاسير:

external-link copy
6 : 75

يَسۡـَٔلُ أَيَّانَ يَوۡمُ ٱلۡقِيَٰمَةِ

Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama? info

Anauliza kwa kuona haiwezi kutokea saa ya Kiyama: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?

التفاسير:

external-link copy
7 : 75

فَإِذَا بَرِقَ ٱلۡبَصَرُ

Basi jicho litapo dawaa! info

Jicho litapo tahayari kwa kufazaika na kushtuka,

التفاسير:

external-link copy
8 : 75

وَخَسَفَ ٱلۡقَمَرُ

Na mwezi utapo patwa! info

Na mwangaza wa mwezi ukapotea,

التفاسير:

external-link copy
9 : 75

وَجُمِعَ ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ

Na likakusanywa jua na mwezi! info

Na jua likakusanyika na mwezi kuchomoza magharibi,

التفاسير:

external-link copy
10 : 75

يَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذٍ أَيۡنَ ٱلۡمَفَرُّ

Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio? info

Mtu hapo atasema: Yako wapi makimbilio kuikimbia hii adhabu?

التفاسير:

external-link copy
11 : 75

كَلَّا لَا وَزَرَ

La! Hapana pa kukimbilia! info

Huachi, ewe mtu, kutafuta makimbilio? Leo huna pa kukimbilia wewe,

التفاسير:

external-link copy
12 : 75

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمُسۡتَقَرُّ

Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu. info

ila kwa Mola wako Mlezi peke yake, ndipo penye matulivu ya waja, Peponi au Motoni.

التفاسير:

external-link copy
13 : 75

يُنَبَّؤُاْ ٱلۡإِنسَٰنُ يَوۡمَئِذِۭ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ

Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha. info

Siku hiyo mtu ataambiwa vitendo vyake alivyo vitanguliza na alivyo viakhirisha.

التفاسير:

external-link copy
14 : 75

بَلِ ٱلۡإِنسَٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٞ

Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake. info

Bali mtu yeye mwenyewe ni hoja iliyo wazi juu ya nafsi yake inayo mkazania kwa anayo yatenda na anayo yaacha.

التفاسير:

external-link copy
15 : 75

وَلَوۡ أَلۡقَىٰ مَعَاذِيرَهُۥ

Na ingawa atatoa chungu ya udhuru. info

Na ijapo kuwa atajitolea chungu nzima ya udhuru na akazieneza, hawezi kabisa kuepukana na hoja hizo.

التفاسير:

external-link copy
16 : 75

لَا تُحَرِّكۡ بِهِۦ لِسَانَكَ لِتَعۡجَلَ بِهِۦٓ

Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka. info

Usiuharikishe ulimi wako kwa kuisoma Qur'ani na kujaribu kuihifadhi kwa haraka pale unapo teremshiwa kwa Wahyi.

التفاسير:

external-link copy
17 : 75

إِنَّ عَلَيۡنَا جَمۡعَهُۥ وَقُرۡءَانَهُۥ

Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. info

Hakika ni juu yetu Sisi kuikusanya hiyo katika kifua chako, na kuithibitisha katika ulimi wako.

التفاسير:

external-link copy
18 : 75

فَإِذَا قَرَأۡنَٰهُ فَٱتَّبِعۡ قُرۡءَانَهُۥ

Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake. info

Akikusomea Mjumbe wetu (Jibril) basi nawe ifuatilize kama unavyo isikia.

التفاسير:

external-link copy
19 : 75

ثُمَّ إِنَّ عَلَيۡنَا بَيَانَهُۥ

Kisha ni juu yetu kuubainisha. info

Kisha baada ya hayo ni juu yetu kuibainisha ikiingia tatizo lolote juu yako.

التفاسير:

external-link copy
20 : 75

كَلَّا بَلۡ تُحِبُّونَ ٱلۡعَاجِلَةَ

Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani, info

Wacheni kukanya kufufuliwa, na hilo ni jambo la kweli. Lakini nyinyi mnaipenda dunia na starehe zake,

التفاسير:

external-link copy
21 : 75

وَتَذَرُونَ ٱلۡأٓخِرَةَ

Na mnaacha maisha ya Akhera. info

Na mnaiacha Akhera na neema zake.

التفاسير:

external-link copy
22 : 75

وُجُوهٞ يَوۡمَئِذٖ نَّاضِرَةٌ

Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara, info

Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.

التفاسير:

external-link copy
23 : 75

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٞ

Zinamwangallia Mola wao Mlezi. info

Siku hiyo zitakuwapo nyuso nzuri, zenye kumwangalia Mola wao Mlezi bila ya kusema kwa sifa gani, wajihi gani, au masafa gani.

التفاسير:

external-link copy
24 : 75

وَوُجُوهٞ يَوۡمَئِذِۭ بَاسِرَةٞ

Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana. info

Na nyuso nyengine zitakuwapo zimenuna, zimekunjana mno, zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.

التفاسير:

external-link copy
25 : 75

تَظُنُّ أَن يُفۡعَلَ بِهَا فَاقِرَةٞ

Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo. info

Zinangojea zitendewe jambo ambalo kwa kitisho chake linavunja uti wa mgongo.

التفاسير:

external-link copy
26 : 75

كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِيَ

La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo, info

Mna nini na kuipenda dunia ambayo mnaifariki roho inapo fika katika mafupa ya kooni,

التفاسير:

external-link copy
27 : 75

وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٖ

Na pakasemwa: Nani wa kumganga? info

Na walio hudhuria wakasema: Yupo wa kumganga huyu kwa haya aliyo nayo?

التفاسير:

external-link copy
28 : 75

وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ

Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki; info

Akayakinisha yule yaliyo mfika mauti kama lililo mshukia ni kuiacha dunia inayo pendwa, na imekwisha mfika shida yake kikomo cha mwisho.

التفاسير:

external-link copy
29 : 75

وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ

Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi, info

Na muundi wa mguu umekwisha ambatana na wa pili wakati wa kutoka roho.

التفاسير:

external-link copy
30 : 75

إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡمَسَاقُ

Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi! info

Kwa Mola wako Mlezi tu siku hiyo ndio machungio ya waja, ama Peponi au Motoni.

التفاسير:

external-link copy
31 : 75

فَلَا صَدَّقَ وَلَا صَلَّىٰ

Kwa sababu hakusadiki, wala hakuswali. info

Binaadamu amekanya kufufuliwa, na kwa hivyo hakumsadiki Mtume wala Qur'ani. Wala hakumtimizia Mwenyezi Mungu faridha za Swala.

التفاسير:

external-link copy
32 : 75

وَلَٰكِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ

Bali alikanusha, na akageuka. info

Lakini aliikadhibisha Qur'ani, akaipuuza Imani,

التفاسير:

external-link copy
33 : 75

ثُمَّ ذَهَبَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ يَتَمَطَّىٰٓ

Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao. info

Na akatoka kwenda kwa watu wake wa nyumbani kwa maringo na kujitapa.

التفاسير:

external-link copy
34 : 75

أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ

Ole wako, ole wako! info

Ewe unaye kadhibisha, utaangamia!

التفاسير:

external-link copy
35 : 75

ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ

Kisha Ole wako, ole wako! info

Tena utaangamia! Na tena utaangamia, na utaangamia!

التفاسير:

external-link copy
36 : 75

أَيَحۡسَبُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَن يُتۡرَكَ سُدًى

Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure? info

Hivyo anadhani huyu mtu anaye kanya kufufuliwa kuwa ataachwa hivi hivi akiringa tu katika maisha yake, na akisha kufa iwe basi, wala asifufuliwe akahisabiwa kwa vitendo vyake?

التفاسير:

external-link copy
37 : 75

أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةٗ مِّن مَّنِيّٖ يُمۡنَىٰ

Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa? info

Kwani yeye mtu hakuwa ni tone tu ya manii, ilio jaaliwa kuwemo katika tumbo la uzazi?

التفاسير:

external-link copy
38 : 75

ثُمَّ كَانَ عَلَقَةٗ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ

Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo. info

Kisha hiyo tone ikawa kipande cha damu iliyo ganda, na Mwenyezi Mungu akaiumba, akaisawazisha mpaka ikawa na umbo zuri?

التفاسير:

external-link copy
39 : 75

فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke. info

Akajaalia namna mbili, mwanamume na mwanamke?

التفاسير:

external-link copy
40 : 75

أَلَيۡسَ ذَٰلِكَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧيَ ٱلۡمَوۡتَىٰ

Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu? info

Je! Huyo Muumba wa mwanzo aliye fanya yote haya, basi si muweza wa kuwahuisha maiti baada ya kuyakusanya mafupa yao?

التفاسير: