ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

Al-Ma'arij

external-link copy
1 : 70

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ

Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea! info

Ameita, mwenye kuita, kuhimiza kama kufanya kejeli, iletwe upesi adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo hapana shaka itawashukia makafiri.

التفاسير:

external-link copy
2 : 70

لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ

Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia . info

Wala hapana chochote cha kuzuia adhabu hiyo,

التفاسير:

external-link copy
3 : 70

مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ

Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. info

Kwani hiyo inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu, ambako huko ndiko zinatoka nguvu zinazo simama, na hukumu inayo tekelezwa.

التفاسير:

external-link copy
4 : 70

تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ

Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! info

Malaika na Jibrili wanapanda kwenda kunako toka amri yake kwa siku ambayo urefu wake ni miaka khamsini elfu kwa mujibu wa hisabu ya miaka ya duniani.

التفاسير:

external-link copy
5 : 70

فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا

Basi subiri kwa subira njema.Hakika wao wanaiona iko mbali! info

Basi, ewe Muhammad! Subiri uwastahamilie hizo kejeli zao, na kuhimiza kwao adhabu, kwa subira isiyo kuwa na mbabaiko ndani yake wala mashtaka.

التفاسير:

external-link copy
6 : 70

إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا

Hakika wao wanaiona iko mbali! info

Hakika hao makafiri wanaiona hiyo Siku ya Kiyama ni kitu cha muhali kutokea.

التفاسير:

external-link copy
7 : 70

وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا

Na Sisi tunaiona iko karibu. info

Na Sisi tunaona kuwa ni jambo jepesi katika uweza wetu, wala halina uzito wowote.

التفاسير:

external-link copy
8 : 70

يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ

Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. info

Siku mbingu itakapo kuwa kama fedha iliyo yayuka,

التفاسير:

external-link copy
9 : 70

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ

Na milima itakuwa kama sufi. info

Na milima itakapo kuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na ikapigwa,

التفاسير:

external-link copy
10 : 70

وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمٗا

Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. info

Wala jamaa hamuulizi jamaa yake: Nini hali yako? Kwa sababu kila mmoja kajishughulikia nafsi yake!

التفاسير:

external-link copy
11 : 70

يُبَصَّرُونَهُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِي مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِئِذِۭ بِبَنِيهِ

Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, info

Watakuwa wakijuulishana wao kwa wao mpaka wajuane baraabara, na ilhali hapana amuulizae mwenzie kitu. Kafiri atatamani lau ange pata kujikomboa nafsi yake na adhabu hiyo Siku ya Kiyama kwa kumtoa mwanawe awe ni fidia yake,

التفاسير:

external-link copy
12 : 70

وَصَٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ

Na mkewe, na nduguye, info

Au mkewe, au nduguye,

التفاسير:

external-link copy
13 : 70

وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِي تُـٔۡوِيهِ

Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, info

Au jamaa zake aliyo khusiana nao,

التفاسير:

external-link copy
14 : 70

وَمَن فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا ثُمَّ يُنجِيهِ

Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. info

Na wote waliomo duniani, apate kuokoka yeye tu!

التفاسير:

external-link copy
15 : 70

كَلَّآۖ إِنَّهَا لَظَىٰ

La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, info

Ewe mkosefu! Wacha hayo unayo yatamani ya kutaka kujikomboa kwa fidia! Hakika huo moto, unawaka kweli!

التفاسير:

external-link copy
16 : 70

نَزَّاعَةٗ لِّلشَّوَىٰ

Unao babua ngozi ya kichwa! info

Utakubabua mikono yako, na miguu yako, na viungo vyako vyote,

التفاسير:

external-link copy
17 : 70

تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ

Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. info

Utanadi kwa jina la huyo aliye iacha Haki, na akaacha ut'iifu,

التفاسير:

external-link copy
18 : 70

وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ

Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. info

Na akakusanya mali akayaweka katika mabweta yake, wala hakutoa haki ya Mwenyezi Mungu iliomo katika hayo mali!

التفاسير:

external-link copy
19 : 70

۞ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا

Hakika mtu ameumbwa na papara. info

Hakika tabia ya binaadamu ni papara, mwingi wa kupapatika,

التفاسير:

external-link copy
20 : 70

إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعٗا

Inapo mgusa shari hupapatika. info

Na kutoridhika akifikiwa na lolote la karaha na uzito,

التفاسير:

external-link copy
21 : 70

وَإِذَا مَسَّهُ ٱلۡخَيۡرُ مَنُوعًا

Na inapo mgusa kheri huizuilia. info

Na ni mwingi wa kuzuia na kunyima akipata kheri na neema.

التفاسير:

external-link copy
22 : 70

إِلَّا ٱلۡمُصَلِّينَ

Isipo kuwa wanao swali, info

Isipo kuwa wanao swali,

التفاسير:

external-link copy
23 : 70

ٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ دَآئِمُونَ

Ambao wanadumisha Sala zao, info

Ambao wanadumisha Swala zao, hawakikosi hata kipindi kimoja.

التفاسير:

external-link copy
24 : 70

وَٱلَّذِينَ فِيٓ أَمۡوَٰلِهِمۡ حَقّٞ مَّعۡلُومٞ

Na ambao katika mali yao iko haki maalumu info

Na wale ambao katika mali yao ipo haki iliyo ainiwa

التفاسير:

external-link copy
25 : 70

لِّلسَّآئِلِ وَٱلۡمَحۡرُومِ

Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; info

iliyo wekwa kwa ajili ya masikini mwenye kuomba kutaka msaada, na anaye jizuilia kuomba pia. (Katika wanao zuilika kuomba wanaingia si wenye kustahi na kuona vibaya tu, bali pia wasio weza kuomba kama watoto wachanga, wagonjwa, na wanyama pia.)

التفاسير:

external-link copy
26 : 70

وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, info

Na wale wanao isadiki Siku ya Malipo, basi wanajitayarisha kwa ajili yake;

التفاسير:

external-link copy
27 : 70

وَٱلَّذِينَ هُم مِّنۡ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشۡفِقُونَ

Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. info

Na wale wanao iogopa adhabu ya Mola wao Mlezi basi wanajikinga nayo wala hawajitii katika jambo la kuwaletea adhabu hiyo.

التفاسير:

external-link copy
28 : 70

إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمۡ غَيۡرُ مَأۡمُونٖ

Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. info

Kwani hakika adhabu ya Mola wao Mlezi hapana hata mmoja anaye weza kuaminika nayo isimpate.

التفاسير:

external-link copy
29 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِفُرُوجِهِمۡ حَٰفِظُونَ

Na ambao wanahifadhi tupu zao. info

Na ambao wanazihifadhi tupu zao hata hawaemewi na matamanio yao.

التفاسير:

external-link copy
30 : 70

إِلَّا عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ فَإِنَّهُمۡ غَيۡرُ مَلُومِينَ

Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi info

Lakini kwa wake zao na masuria wao hawazihifadhi; kwa sababu hapo hawalaumiwi kuifuata tabia ya maumbile.

التفاسير:

external-link copy
31 : 70

فَمَنِ ٱبۡتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡعَادُونَ

Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. info

Basi mwenye kutafuta starehe ya maingiliano kwa wasio kuwa wake na masuria, basi hao tena ni wenye kuikiuka halali na kuingia katika haramu.

التفاسير:

external-link copy
32 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ لِأَمَٰنَٰتِهِمۡ وَعَهۡدِهِمۡ رَٰعُونَ

Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, info

Na hao wenye kuzihifadhi amana za sharia na amana za waja wa Mwenyezi Mungu, na walio lazimika nayo kwa Mwenyezi Mungu na kwa watu bila ya kukhuni wala kupunja,

التفاسير:

external-link copy
33 : 70

وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَٰدَٰتِهِمۡ قَآئِمُونَ

Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, info

Na ambao kwa shahada zao wamesimama sawa sawa kwa haki bila ya kuficha wanalo lijua,

التفاسير:

external-link copy
34 : 70

وَٱلَّذِينَ هُمۡ عَلَىٰ صَلَاتِهِمۡ يُحَافِظُونَ

Na ambao wanazihifadhi Sala zao. info

Na wanao hifadhi Swala zao wakizisali sawasawa kwa ukamilifu -

التفاسير:

external-link copy
35 : 70

أُوْلَٰٓئِكَ فِي جَنَّٰتٖ مُّكۡرَمُونَ

Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. info

Watu wenye sifa kama hizo nzuri watakuwa ni wenye kuhishimiwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu huko Peponi.

التفاسير:

external-link copy
36 : 70

فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ قِبَلَكَ مُهۡطِعِينَ

Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? info

Kitu gani kinawapelekea hao walio kufuru kukujia mbio mbio ?

التفاسير:

external-link copy
37 : 70

عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ

Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! info

Kutoka kuliani na kushotoni kwa makundi?

التفاسير:

external-link copy
38 : 70

أَيَطۡمَعُ كُلُّ ٱمۡرِيٕٖ مِّنۡهُمۡ أَن يُدۡخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٖ

Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? info

Je, kwani kila mmoja wao ana tamaa ya kuingia kwenye Pepo yenye neema, baada ya kusikia kuwa Mwenyezi Mungu amemuahidi Mtume wake na Waumini kuwatia Peponi?

التفاسير:

external-link copy
39 : 70

كَلَّآۖ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّمَّا يَعۡلَمُونَ

La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. info

Basi nawaache hiyo tamaa yao ya kuingia Peponi. Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na maji ya kudharauliwa.

التفاسير:

external-link copy
40 : 70

فَلَآ أُقۡسِمُ بِرَبِّ ٱلۡمَشَٰرِقِ وَٱلۡمَغَٰرِبِ إِنَّا لَقَٰدِرُونَ

Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza info

Naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote, na magharibi zote za siku, na sayari na hidaya, kwamba hakika bila ya shaka Sisi tuna uweza wa kuwaangamiza,

التفاسير:

external-link copy
41 : 70

عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ

Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. info

Na kuwaleta walio wat'iifu zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao. Wala Sisi hatushindwi kubadilisha huko. Huenda ikawa inakusudiwa kwa "mashariki zote" na "magharibi zote" ni maeneo ya mamlaka ya Mwenyezi Mungu yote ambayo hayana mpaka kama ilivyo ashiriwa katika Aya 137 ya Surat Al-A'araf: "Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki za nchi na magharibi zake ambayo tuliitia baraka", kuonyesha sehemu zote za hiyo nchi inayo tajwa. Na huenda ikawa makusudio yake ni mashariki za jua na mwezi na nyota zote na sayari, na magharibi zao, kwa ajili ya kuonyesha vile vile ufalme wa Mwenyezi Mungu wote. Na kwa hivyo inadhihirika kwetu kuwa vyombo vinavyo kwenda katika qubba la mbingu vinachomoza kwenye upeo wa mashariki na kuchwa kwenye upeo wa magharibi, au kwa uchache vinazunguka kutoka mashariki kwendea magharibi kuizunguka nyota ya Pole, katika sehemu ya kaskazini ya dunia. Kwani umbali wa Pole kwa nyota ni mdogo kuliko pahala unapo angalia, basi nyota hapo haichomozi wala haichwi, bali hupiga duru ndogo kuizunguka North Pole. Na kwa hiyo Aya inaashiria saa za usiku. Rejea kwenye kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: " Na alama na kwa nyota wao wanaongoka." Na kwa udhaahiri wa kuchomoza na kuchwa ipo ishara ya kuzunguka kwa dunia, na hiyo ni neema kubwa kabisa katika neema za Mwenyezi Mungu juu ya maisha katika sayari hii. Kwani bila ya kuzunguka kwa dunia juu ya msumari-kati wake nusu ya dunia ingeli pigwa na jua mfululizo muda wa nusu mwaka kaamili, na ingeli nyimwa mwangaza kabisa nusu nyengine. Kwa hivyo uhai kama tulivyo uzoea usinge kuwako. Na tukifanya hizo mashariki na hizo magharibi ni za jua peke yake, wachilia mbali nyota nyengine na sayari, basi itakuwa ishara ni kule kuchomoza jua kila siku pahala pengine na kuchwa pahala pengine kila siku, au hata katika kila dakika linapo pita juu ya dunia. Kwani jua kila dakika linakuchwa pahala na linachomoza pahala papili mfululizo. Na haya ni katika mipango ya Mwenyezi Mungu na miujiza ya uweza wake. Tazama pia maoni ya wataalamu juu ya Aya ya 5 katika Surat Assaffat, na Aya 17 ya Surat Arrah'man.

التفاسير:

external-link copy
42 : 70

فَذَرۡهُمۡ يَخُوضُواْ وَيَلۡعَبُواْ حَتَّىٰ يُلَٰقُواْ يَوۡمَهُمُ ٱلَّذِي يُوعَدُونَ

Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, info

Basi waachilie wakiporojoka katika upotovu wao, na wakicheza na dunia yao, mpaka wakutane na siku yao waliyo ahidiwa kupewa adhabu.

التفاسير:

external-link copy
43 : 70

يَوۡمَ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ سِرَاعٗا كَأَنَّهُمۡ إِلَىٰ نُصُبٖ يُوفِضُونَ

Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, info

Siku watakapo tolewa makaburini mbio mbio kumwendea huyo ataye waita, kama kwamba wamemweka ufundo na wakimuabudu duniani walivyo kuwa wakimkimbilia badala ya Mwenyezi Mungu,

التفاسير:

external-link copy
44 : 70

خَٰشِعَةً أَبۡصَٰرُهُمۡ تَرۡهَقُهُمۡ ذِلَّةٞۚ ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلَّذِي كَانُواْ يُوعَدُونَ

Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. info

Macho yameinama chini, hawawezi kuyanyanyua, yamegubikwa na unyonge na udhalili. Hiyo ndiyo siku waliyo kuwa wakiahidiwa duniani na wao wakiikanusha.

التفاسير: