ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
2 : 3

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ

Mwenyezi Mungu, hakuna mungu ila Yeye Aliye Hai, Msimamizi wa yote milele. info

Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na kila kiliomo ulimwenguni kinashuhudia hayo kwa namna ya kilivyo umbika na kushikamana, katika umbo na kazi, na viumbe vyenginevyo. Na Yeye Mwenyezi Mungu ni Yuhai, hafi. Ni Mwenye kusimamia na kuendesha mambo yote ya ulimwengu. Yeye ndiye Mwenye kuyadabiri (kuyaendesha) na kuyasarifu.

التفاسير: