ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
126 : 3

وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشۡرَىٰ لَكُمۡ وَلِتَطۡمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِۦۗ وَمَا ٱلنَّصۡرُ إِلَّا مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara kwenu, na ili nyoyo zenu zipate kutua. Na msaada hautoki isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu, Aliye tukuka, Mwenye nguvu na Mwenye hikima. info

Na wala Mwenyezi Mungu hakujaalia huko kukuleteeni msaada wa Malaika ila iwe ni bishara tu kwenu ya ushindi, na zipate kutulia nyoyo zenu. Na hapana ushindi ila unao tokana na Mwenyezi Mungu Mwenye Kushinda wote, ambaye anapanga kila kitu kwa pahala pake, na anaye wapangia mambo waja wake Waumini.

التفاسير: