ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
64 : 22

لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ

Ni vyake viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Mwenye kusifiwa. info

Kila kiliomo mbinguni na katika ardhi ni chake Yeye, na kinamtumikia Yeye peke yake, na anakiendesha kama apendavyo. Na Yeye hawahitajii waja wake, bali wao ndio wanao mhitajia Yeye. Na Yeye ndiye anaye stahiki peke yake kuhimidiwa na kusifiwa na viumbe vyote.

التفاسير: