ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
105 : 21

وَلَقَدۡ كَتَبۡنَا فِي ٱلزَّبُورِ مِنۢ بَعۡدِ ٱلذِّكۡرِ أَنَّ ٱلۡأَرۡضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ ٱلصَّٰلِحُونَ

Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema. info

Na tulikwisha andika katika Zaburi - nacho ni Kitabu cha Daud baada ya Taurati - kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeza, na kusahilisha njia za maisha bora humo. ("Bali wenye upole watairithi nchi"..Zaburi 37.11 "Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele".. Zaburi 37.29)

التفاسير: