ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
73 : 21

وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَئِمَّةٗ يَهۡدُونَ بِأَمۡرِنَا وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِمۡ فِعۡلَ ٱلۡخَيۡرَٰتِ وَإِقَامَ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءَ ٱلزَّكَوٰةِۖ وَكَانُواْ لَنَا عَٰبِدِينَ

Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende kheri, na washike Swala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu. info

Na tukawafanya ni Manabii wakiwaendea watu, wakiwaongoa kwenye kheri kwa mujibu wa tulivyo waamrisha. Na tukawaonyesha vitendo vyema, na kudumisha Swala kama inavyo faa, na kutoa Zaka. Na wakawa wanatunyenyekea na kutusafia ibada Sisi tu.

التفاسير:

external-link copy
74 : 21

وَلُوطًا ءَاتَيۡنَٰهُ حُكۡمٗا وَعِلۡمٗا وَنَجَّيۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَت تَّعۡمَلُ ٱلۡخَبَٰٓئِثَۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمَ سَوۡءٖ فَٰسِقِينَ

Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu. info

Luut'i tukampa kauli ya kukata na madhubuti katika hukumu na ilimu yenye manufaa. Na tukamwokoa kutokana na mji ambao watu wake wanafanya kitendo cha namna ya peke yake katika uovu. Hakika hao walikuwa watu walio shikilia kufanya maovu, walio toka kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu na tabia iliyo zowewa.

التفاسير:

external-link copy
75 : 21

وَأَدۡخَلۡنَٰهُ فِي رَحۡمَتِنَآۖ إِنَّهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa watenda mema. info

Tukampeleka njia ya watu wa rehema yetu. Hakika huyo alikuwa miongoni mwa watu wema alio wakusanya Mwenyezi Mungu katika rehema yake na akawakunjulia msaada wake.

التفاسير:

external-link copy
76 : 21

وَنُوحًا إِذۡ نَادَىٰ مِن قَبۡلُ فَٱسۡتَجَبۡنَا لَهُۥ فَنَجَّيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥ مِنَ ٱلۡكَرۡبِ ٱلۡعَظِيمِ

Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa. info

Na hapa tumjaje Nu'h kabla ya Ibrahim na Luu't, pale alipo muomba Mola wake Mlezi, aisafishe nchi kwa kuondoa waovu tukamuitikia ombi lake, tukamuokowa yeye na wale walioamini katika watu wake, kutokana na shakawa (shida) ya kimbunga kikubwa.

التفاسير:

external-link copy
77 : 21

وَنَصَرۡنَٰهُ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمَ سَوۡءٖ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote. info

Tukamlinda kwa nusura yetu na vitimbi vya kaumu yake walio zikanusha Ishara zetu zenye kuthibitisha Utume wake. Hakika hao walikuwa watu wa shari. Basi tukawagharikisha wote!

التفاسير:

external-link copy
78 : 21

وَدَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ إِذۡ يَحۡكُمَانِ فِي ٱلۡحَرۡثِ إِذۡ نَفَشَتۡ فِيهِ غَنَمُ ٱلۡقَوۡمِ وَكُنَّا لِحُكۡمِهِمۡ شَٰهِدِينَ

Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo. info

Ewe Nabii! Wataje Daud na Suleiman walipo toa hukumu katika kesi ya konde, ilio ingiliwa na mbuzi wa watu mbali usiku na wakala mazao yake. Na Sisi tulikuwa tunaijua hukumu iliyo khusiana na kesi hiyo. Kisa cha hiyo hukumu: Mbuzi waliingia usiku mmoja katika konde ya mtu, wasibakishe kitu. Daud akahukumu kuwa wale mbuzi wawe wa mwenye konde kulipia khasara yake. Suleiman akatoa hukumu nyengine, akasema: Mbuzi wale wabakie mkononi mwa mwenye konde mpaka itapo mea tena mazao yake, na avumilie kwa yaliyo mpata. Na baada yake warejesheane.

التفاسير:

external-link copy
79 : 21

فَفَهَّمۡنَٰهَا سُلَيۡمَٰنَۚ وَكُلًّا ءَاتَيۡنَا حُكۡمٗا وَعِلۡمٗاۚ وَسَخَّرۡنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلۡجِبَالَ يُسَبِّحۡنَ وَٱلطَّيۡرَۚ وَكُنَّا فَٰعِلِينَ

Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo. info

Basi tulimfahamisha Suleiman hiyo fatwa. Na wote wawili tuliwapa hikima na ilimu ya maisha na mambo yake. Na tulimfanyia Daud pamoja na milima it'ii na imtakase Mwenyezi Mungu kama alivyo kuwa anamtakasa yeye Daud na kila lisio kuwa linamwelekea Mwenyezi Mungu. Na kadhaalika tuliwafanya ndege hivyo hivyo wamsabihi Mwenyezi Mungu pamoja naye. Na tulifanya hayo kwa uweza wetu usio shindika.

التفاسير:

external-link copy
80 : 21

وَعَلَّمۡنَٰهُ صَنۡعَةَ لَبُوسٖ لَّكُمۡ لِتُحۡصِنَكُم مِّنۢ بَأۡسِكُمۡۖ فَهَلۡ أَنتُمۡ شَٰكِرُونَ

Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika kupigana kwenu. Je! Mtakuwa wenye kushukuru? info

Tukamfundisha Daud kufuma nguo za chuma, ili zikulindeni katika vita vyenu. Basi mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa neema hii aliyo kuneemesheni.

التفاسير:

external-link copy
81 : 21

وَلِسُلَيۡمَٰنَ ٱلرِّيحَ عَاصِفَةٗ تَجۡرِي بِأَمۡرِهِۦٓ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيۡءٍ عَٰلِمِينَ

Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyo ibarikia. Na Sisi ndio tunao jua kila kitu. info

Na tulimsahilishia Suleiman upepo unao vuma kwa nguvu umtumikie, nao huo ulikuwa unakwenda kwa kufuata amri yake mpaka kwenye nchi tuliyo izidishia kheri yake. Nasi ni wenye kuyajua yote hayo. Halitupotei kubwa wala dogo.

التفاسير: