ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
94 : 2

قُلۡ إِن كَانَتۡ لَكُمُ ٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ عِندَ ٱللَّهِ خَالِصَةٗ مِّن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Ikiwa nyumba ya Akhera iliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni yenu tu bila ya watu wengine, basi tamanini mauti kama nyinyi mnasema kweli. info

Na nyinyi mmedai kuwa Mwenyezi Mungu atakupeni nyinyi tu neema za Pepo baada ya kufa, wasipate watu wote wengineo. Ikiwa basi kweli mnaamini hayo myasemayo basi yafaa myapende mauti. Hebu yatamanini myapate upesi zisije kutaakhari hizo starehe mnazodai.

التفاسير: