ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
39 : 13

يَمۡحُواْ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ وَيُثۡبِتُۖ وَعِندَهُۥٓ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ

Mwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na asili ya hukumu zote iko kwake. info

Mwenyezi Mungu hufuta sharia na miujiza, na akaleta badala yake atakayo na akaithibitisha. Na kwake Yeye ipo asili ya Sharia zilizo thibiti zisio geuka, na ndio kwenye Umoja na asili ya fadhila zote, na mengineyo.

التفاسير: