ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - អាលី ម៉ុហសុីន អាល់ពើវ៉ានី

external-link copy
105 : 11

يَوۡمَ يَأۡتِ لَا تَكَلَّمُ نَفۡسٌ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦۚ فَمِنۡهُمۡ شَقِيّٞ وَسَعِيدٞ

Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja ila kwa idhini yake Mwenyezi Mungu. Kati yao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha. info

Kikija kitisho chake mwanaadamu hatoweza kusema ila kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu. Kwani miongoni mwa watu wapo wenye mashaka, dhiki, wasio na bahati kwa kila namna ya shida watazo pata. Hao ndio makafiri. Na wengine wenye furaha, walio bahatika, kwa neema zinazo wangojea Akhera. Hao ndio Waumini.

التفاسير: