ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

Az-Zalzalah

external-link copy
1 : 99

إِذَا زُلۡزِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ زِلۡزَالَهَا

Itakapotikiswa ardhi mtikiso wa nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 99

وَأَخۡرَجَتِ ٱلۡأَرۡضُ أَثۡقَالَهَا

Na ikatoa vilivyomo ndani yake: wafu na makandi. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 99

وَقَالَ ٱلۡإِنسَٰنُ مَا لَهَا

Na akauliza binadamu, kwa babaiko, «Imezukiwa na nini?» info
التفاسير:

external-link copy
4 : 99

يَوۡمَئِذٖ تُحَدِّثُ أَخۡبَارَهَا

Siku ya Kiyama ardhi itatoa habari ya mambo iliyofanyiwa ya uzuri na ubaya. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 99

بِأَنَّ رَبَّكَ أَوۡحَىٰ لَهَا

kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ameiamuru itoe habari ya mambo iliyofanyiwa. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 99

يَوۡمَئِذٖ يَصۡدُرُ ٱلنَّاسُ أَشۡتَاتٗا لِّيُرَوۡاْ أَعۡمَٰلَهُمۡ

Siku hiyo wataondoka kutoka kwenye kisimamo cha Hesabu wakiwa makundi, ili Mwenyezi Mungu Awaoneshe waliyoyatenda, mazuri na mabaya, na Awalipe kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 99

فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرٗا يَرَهُۥ

Yoyote mwenye kufanya jema wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 99

وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ شَرّٗا يَرَهُۥ

Na yoyote mwenye kufanya baya wezani wa chungu mdogo atayaona malipo yake Akhera. info
التفاسير: