ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

Al-Lail

external-link copy
1 : 92

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ

Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 92

وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ

Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 92

وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ

Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike, info
التفاسير:

external-link copy
4 : 92

إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ

Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 92

فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ

Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa, info
التفاسير:

external-link copy
6 : 92

وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ

akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo, info
التفاسير:

external-link copy
7 : 92

فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ

Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 92

وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ

Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 92

وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ

akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo, info
التفاسير: