ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
19 : 74

فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ

Hivyo basi akalaaniwa na akastahili, kwa hilo, maangamivu: alijiandaa vipi ndani ya nafsi yake kwa hayo matukano? info
التفاسير:

external-link copy
20 : 74

ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ

Kisha pia akalaaniwa. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 74

ثُمَّ نَظَرَ

Kisha yeye alifikiria kuhusu kile alichokipanga na kukitayarisha cha kuitia dosari Qur’ani. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 74

ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ

Kisha akafinya uso wake na akazidi katika hali ile ya ukunjaji uso kwa kukosa hila za kufanya na kutopata ila yoyote ya kuitia dosari Qur’ani. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 74

ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ

Kisha akarudi kuipa mgongo haki na akajiona ni mkubwa wa kutofaa kuikubali, info
التفاسير:

external-link copy
24 : 74

فَقَالَ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ يُؤۡثَرُ

hapo akasema kuhusu Qur’ani, «Haya anayoyasema Muhammad si chochote isipokuwa ni uchawi uliopokewa kutoka kwa watu wa mwanzo waliopita. info
التفاسير:

external-link copy
25 : 74

إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ

Haikuwa hi Qur’ani isipokuwa ni maneno ya viumbe ambayo Muhammad amejifunza kutoka kwao kisha akadai kuwa yanatoka kwa Mwenyezi Mungu.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 74

سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ

Basi nitamuingiza kwenye moto wa Jahanamu ili alionje joto lake na achomeke kwa moto wake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 74

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سَقَرُ

Na ni lipi lililokujulisha wewe ni kitu gani hiyo Jahanamu? info
التفاسير:

external-link copy
28 : 74

لَا تُبۡقِي وَلَا تَذَرُ

Haibakishi nyama wala haiachi mfupa isipokuwa huvichoma. info
التفاسير:

external-link copy
29 : 74

لَوَّاحَةٞ لِّلۡبَشَرِ

Unageuza ngozi ya mwili, unazifanya ngozi kuwa nyeusi na unazichoma. info
التفاسير:

external-link copy
30 : 74

عَلَيۡهَا تِسۡعَةَ عَشَرَ

Wanasimamia mambo yake na kushikilia kazi ya kuwatesa watu wake Malaika kumi na tisa katika washika zamu wa Motoni wenye nguvu. info
التفاسير:

external-link copy
31 : 74

وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَٰٓئِكَةٗۖ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَهُمۡ إِلَّا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَٰنٗا وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلٗاۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ

Na hatukuwafanya washika hazina wa Motoni isipokuwa miongoni mwa Malaika washupavu. Na hatukuiweka idadi hiyo isipokuwa kuwatahini wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na ili imani ya yakini ipatikane kwa wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu kwamba yaliyokuja ndani ya Qur’ani juu ya washika hazina wa Motoni ni ukweli utokao kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, kwani hayo yanaafikiana na vitabu vyao, na ili Waumini wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na waifuate Sheria Yake kivitendo, na ili wasilifanyie shaka hilo wale Mayahudi na Wanaswara waliopewa Vitabu wala wale wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na ili wapate kusema wale wenye unafiki ndani ya nyoyo zao na makafiri, «Ni lipi alilolikusudia Mwenyezi Mungu kwa idadi hii ya ajabu?» Kwa mfano wa hayo yaliyotajwa, Mwenyezi Mungu Anampoteza Anayetaka kumpoteza na Anamuongoza Anayetaka kumuongoza. Na hakuna ajuwaye idadi ya askari wa Mola wako, na miongoni mwao ni Malaika, isipokuwa Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na haukuwa huu Moto isipokuwa ni ukumbusho na mazingatio kwa watu. info
التفاسير:

external-link copy
32 : 74

كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ

Mambo sivyo kama walivyotaja ya ukanushaji Mtume katika yale aliyokuja nayo! Anaapa Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, kwa mwezi, info
التفاسير:

external-link copy
33 : 74

وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ

na kwa usiku unapogeuka kwenda zake, info
التفاسير:

external-link copy
34 : 74

وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ

na kwa asubuhi inapotoa mwangaza na kufunuka, info
التفاسير:

external-link copy
35 : 74

إِنَّهَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ

hakika Moto ni mojawapo ya mambo makubwa, info
التفاسير:

external-link copy
36 : 74

نَذِيرٗا لِّلۡبَشَرِ

kwa ajili ya kuwaonya na kuwatisha watu, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 74

لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ

kwa anayetaka miongoni mwenu kujiweka karibu na Mola wake kwa kufanya matendo ya utiifu, au kujikalisha nyuma kwa kufanya matendo ya uasi. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 74

كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ

Kila nafsi imefungwa na kuwekwa rahani kwa ilichokitenda, miongoni mwa matendo mema au mabaya, kwa kukichuma. Haifunguliwi mpaka itekeleze haki zilizo juu ya lazima yake na ipatiwe mateso yanayostahili kupatiwa. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 74

إِلَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلۡيَمِينِ

Isipokuwa Waislamu waliotakaswa, watu wa upande wa kulia waliojikomboa shingo zao kwa utiifu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 74

فِي جَنَّٰتٖ يَتَسَآءَلُونَ

Wao watakuwa kwenye mabustani ya Peponi ambayo sifa zake hazifikiwi ukomo. Watakuwa wakiulizana wao kwa wao info
التفاسير:

external-link copy
41 : 74

عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ

kuhusu makafiri waliojikosea nafsi zao, info
التفاسير:

external-link copy
42 : 74

مَا سَلَكَكُمۡ فِي سَقَرَ

«Ni lipi lililowaingiza kwenye moto wa Jahanamu na likawafanya info
التفاسير:

external-link copy
43 : 74

قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ

mlionje joto lake lililo kali sana?» Wahalifu waseme , «Hatukuwa ni miongoni mwa wanaoswali duniani, info
التفاسير:

external-link copy
44 : 74

وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ

na hatukuwa tukitoa sadaka na kuwafanyia wema wahitaji na maskini, info
التفاسير:

external-link copy
45 : 74

وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآئِضِينَ

na tulikuwa tukizungumza maneno ya ubatilifu na watu wa upotofu na upotevu, info
التفاسير:

external-link copy
46 : 74

وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ

na tulikuwa tukiikanusha Siku ya kuhesabiwa na kulipwa, info
التفاسير:

external-link copy
47 : 74

حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلۡيَقِينُ

mpaka kifo kikatujia na hali sisi tuko kwenye mambo hayo mabaya ya upotevu. info
التفاسير: