ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
14 : 72

وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا

«Na kwamba miongoni mwetu kuna wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa kumtii, na miongoni mwetu kuna waliopotoka walio madhalimu ambao walienda kombo na njia ya haki. Basi mwenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kwa utiifu, hao ndio walioelekea njia ya haki na usawa, wakajibidiisha kuichagua na Mwenyezi Mungu Akawaongoza kuifikia. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 72

وَأَمَّا ٱلۡقَٰسِطُونَ فَكَانُواْ لِجَهَنَّمَ حَطَبٗا

Ama wale waliopotoka na njia ya Uislamu, watakuwa ni kuni za Moto wa Jahanamu.» info
التفاسير:

external-link copy
16 : 72

وَأَلَّوِ ٱسۡتَقَٰمُواْ عَلَى ٱلطَّرِيقَةِ لَأَسۡقَيۡنَٰهُم مَّآءً غَدَقٗا

Na lau makafiri wa kibinadamu na kijini wangalifuata njia ya Uislamu na wasijiepushe nayo, tungaliwateremshia maji mengi na tungaliwakunjulia riziki duniani, info
التفاسير:

external-link copy
17 : 72

لِّنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَمَن يُعۡرِضۡ عَن ذِكۡرِ رَبِّهِۦ يَسۡلُكۡهُ عَذَابٗا صَعَدٗا

ili tuwafanyie mtihani: vipi watazishukuru neema za Mwenyezi Mungu juu yao? Na yoyote mwenye kupa mgongo utiifu wa Mwenyezi Mungu na kusikiliza Qur’ani na kuizingatia na kuifuata kivitendo, Mwenyezi Mungu Atamuingiza kwenye adhabu kali iliyo ngumu. info
التفاسير:

external-link copy
18 : 72

وَأَنَّ ٱلۡمَسَٰجِدَ لِلَّهِ فَلَا تَدۡعُواْ مَعَ ٱللَّهِ أَحَدٗا

Na kwa hakika misikiti ni ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu Peke Yake, basi msiabudu humo asiyekuwa Yeye. Na mtakasieni maombi na ibada humo, kwani misikiti haikujengwa isipokuwa kwa ajili Mwenyezi Mungu Aabudiwe humo Peke Yake, na sio mwingine asiyekuwa Yeye. Katika haya kuna ulazima wa kuiepusha misikiti na kila kinachokoroga utakasaji wa Mwenyezi Mungu na ufuataji Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 72

وَأَنَّهُۥ لَمَّا قَامَ عَبۡدُ ٱللَّهِ يَدۡعُوهُ كَادُواْ يَكُونُونَ عَلَيۡهِ لِبَدٗا

Na kwa hakika Aliposimama Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kumuabudu Mola wake, walikaribia majini kumwangukia wakiwa makundi yaliyojikusanya na kupandana kwa kusongamana sana ili wapate kuisikia Qur’ani kutoka kwake info
التفاسير:

external-link copy
20 : 72

قُلۡ إِنَّمَآ أَدۡعُواْ رَبِّي وَلَآ أُشۡرِكُ بِهِۦٓ أَحَدٗا

Waambie, ewe Mtume, hawa makafiri, «Kwa hakika mimi ninamuabudu Mola wangu Peke Yake, wala simshirikishi na Yeye kitu chochote katika kuabudu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 72

قُلۡ إِنِّي لَآ أَمۡلِكُ لَكُمۡ ضَرّٗا وَلَا رَشَدٗا

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa makafiri, «Mimi siwezi kuwaondolea shida yoyote wala kuwaletea manufaa yoyote.» info
التفاسير:

external-link copy
22 : 72

قُلۡ إِنِّي لَن يُجِيرَنِي مِنَ ٱللَّهِ أَحَدٞ وَلَنۡ أَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلۡتَحَدًا

Sema, «Hakika mimi sina yoyote wa kuniokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu iwapo nitamuasi, na sitapata asiyekuwa Yeye mahali pa kukimbilia niepukane na adhabu Yake. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 72

إِلَّا بَلَٰغٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِسَٰلَٰتِهِۦۚ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا

Ninachokiweza mimi na kukimiliki ni kuwafikishia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kile Alichoniamrisha niwafikishie na ujumbe Wake ambao Alinituma niwaletee. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na akaipa mgongo Dini ya Mwenyezi Mungu, basi malipo yake ni moto wa Jahanamu ambao hatatoka humo milele. info
التفاسير:

external-link copy
24 : 72

حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ أَضۡعَفُ نَاصِرٗا وَأَقَلُّ عَدَدٗا

Mpaka watakapoishuhudia washirikina adhabu anayoahidiwa, hapo watajua itakapowashukia wao: ni nani ambaye mtetezi wake na msaidizi ni mnyonge zaidi na ambaye askari wake ni wachache zaid? info
التفاسير:

external-link copy
25 : 72

قُلۡ إِنۡ أَدۡرِيٓ أَقَرِيبٞ مَّا تُوعَدُونَ أَمۡ يَجۡعَلُ لَهُۥ رَبِّيٓ أَمَدًا

Waambie hawa washirikina, ewe Mtume, Mimi sijui: Je adhabu hii mliyoahidiwa zishakaribia zama zake au Mola wangu ataufanya muda wake wa kuja uwe mrefu? info
التفاسير:

external-link copy
26 : 72

عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ فَلَا يُظۡهِرُ عَلَىٰ غَيۡبِهِۦٓ أَحَدًا

Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, ni mjuzi wa kisichoonekana na macho. Hatakitoa wazi hiko kisichoonekana kwa yoyote miongoni mwa viumbe Wake. info
التفاسير:

external-link copy
27 : 72

إِلَّا مَنِ ٱرۡتَضَىٰ مِن رَّسُولٖ فَإِنَّهُۥ يَسۡلُكُ مِنۢ بَيۡنِ يَدَيۡهِ وَمِنۡ خَلۡفِهِۦ رَصَدٗا

Isipokuwa kwa yule Aliyemchagua Mwenyezi Mungu na kumpendelea kwa kumpa utume, kwani Yeye huwajuza baadhi ya yale yaliyofichika yasionekane. Na Anatuma, mbele ya huyo Mtume na nyuma yake, Malaika wenye kumhifadhi na majini, ili wasiisikilize kwa kuiba jambo hilo la ghaibu, kisha wakaambiana kwa siri kisha wakawadokeza makuhani. info
التفاسير:

external-link copy
28 : 72

لِّيَعۡلَمَ أَن قَدۡ أَبۡلَغُواْ رِسَٰلَٰتِ رَبِّهِمۡ وَأَحَاطَ بِمَا لَدَيۡهِمۡ وَأَحۡصَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ عَدَدَۢا

Ili Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, ajue kwamba Mitume kabla yake walikuwa kwenye hali kama yake ya ufikishaji haki na ukweli, na kwamba yeye atalindwa kutokana na majini kama walivyolindwa wao, na kwamba Mwenyezi Mungu, ujuzi Wake umeyazunguka mambo yao waliyonayo ya nje na ya ndani, miongoni mwa sheria na hukumu na mengineyo, hakuna chochote kinachompita katika hayo, na kwamba Yeye Amekidhibiti kila kitu kwa hesabu, hakuna chochote kinachofichamana Kwake. info
التفاسير: