ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
5 : 63

وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ

Na wanapoambiwa hawa wanafiki, «Njooni huku hali ya kutubia mtake udhuru wa hayo yaliyotokea kwenu ya maneno maovu na mazungumzo ya ufidhuli, ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zenu , huvigeuza vichwa vyao na wakavitikisa kwa njia ya shere na kiburi. Na utawaona, ewe Mtume, wanakupa mgongo na huku wao wanalifanyia kiburi jambo la kufuata yale ambayo walitakiwa wayafuate. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 63

سَوَآءٌ عَلَيۡهِمۡ أَسۡتَغۡفَرۡتَ لَهُمۡ أَمۡ لَمۡ تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ لَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Yanalingana kwa wanafiki hawa, uwaombee msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ewe Mtume, au usiwaombee, kwani Mwenyezi Mungu Hatazisamehe dhambi zao kabisa kwa sababu ya kuendelea kwao na uasi na kujikita kwao kwenye ukafiri. Hakika Mwenyezi Mungu Hawaelekezi kwenye Imani watu wanaomkanusha waliotoka nje ya utiifu Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 63

هُمُ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُواْ عَلَىٰ مَنۡ عِندَ رَسُولِ ٱللَّهِ حَتَّىٰ يَنفَضُّواْۗ وَلِلَّهِ خَزَآئِنُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَفۡقَهُونَ

Wanafiki hawa ndio wao wanaosema kuwaambia watu wa Madina, «Msitoe kuwasaidia Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu waliohama mpaka wajiepushe naye.» Ni za Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hazina za mbinguni na ardhini na vilivyomo humo miongoni mwa riziki, Humpa Anayemtaka na Humnyima Anayemtaka, lakini wanafiki hawaelewi kwamba riziki inatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ujinga wao wa kutomjua Yeye, kutakasika na kila upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 63

يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعۡنَآ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ لَيُخۡرِجَنَّ ٱلۡأَعَزُّ مِنۡهَا ٱلۡأَذَلَّۚ وَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِۦ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَلَٰكِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ لَا يَعۡلَمُونَ

Wanasema hawa wanafiki, «Tutakaporudi Madina, kundi letu lenye nguvu zaidi litalitoa kundi la Waumini lililo twevu zaidi.» Kwa hakika, nguvu na ushindi ni vya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni vya Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na ni vya wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, si vya wale wasiokuwa wao, lakini wanafiki hawalijui hilo kwa ujinga wao uliokita mizizi. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 63

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تُلۡهِكُمۡ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡ عَن ذِكۡرِ ٱللَّهِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Yasiwashughulishe nyinyi mali yenu wala wana wenu na kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii. Na yoyote atakayeshughulishwa na mali Yake na watoto Wake na hilo la kumuabudu Mwenyezi Mungu, basi hao ndio waliopunjwa hisa zao za makaribisho ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 63

وَأَنفِقُواْ مِن مَّا رَزَقۡنَٰكُم مِّن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنِيٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na toeni, enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu.» info
التفاسير:

external-link copy
11 : 63

وَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَاۚ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ

Na wala Mwenyezi Mungu hatoichelewesha nafsi yoyote utakapokuja wakati wa kifo chake na umri wake ukakoma. Na Mwenyezi Mungu, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake, ni mtambuzi wa yale mnayoyatenda: mema na mabaya, na Awetawalipa nyinyi kwa hayo. info
التفاسير: