ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
9 : 62

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, endeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha nyinyi na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu nyinyi kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.Basi iwapo nyinyi mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo. Kwenye aya hii kuna dalili kwamba kwenda kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 62

فَإِذَا قُضِيَتِ ٱلصَّلَوٰةُ فَٱنتَشِرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَٱبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِ ٱللَّهِ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ

Basi mkisha kuisikia hutuba na mkaitekeleza Swala, tawanyikeni kwenye ardhi na mtafute riziki ya Mwenyezi Mungu kwa kwenda mbio kwenu, na mtajeni Mwenyezi Mungu kwa wingi katika hali zenu zote, ili mfaulu kuzipata kheri mbili: za duniani na za Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
11 : 62

وَإِذَا رَأَوۡاْ تِجَٰرَةً أَوۡ لَهۡوًا ٱنفَضُّوٓاْ إِلَيۡهَا وَتَرَكُوكَ قَآئِمٗاۚ قُلۡ مَا عِندَ ٱللَّهِ خَيۡرٞ مِّنَ ٱللَّهۡوِ وَمِنَ ٱلتِّجَٰرَةِۚ وَٱللَّهُ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Na pindi wanapoona baadhi ya Waislamu biashara au chochote miongoni mwa viliwazo vya duniani na pambo lake, hutawanyika kwenda huko na wakakuacha wewe umesimama juu ya mimbari unatoa hutuba. Waambie, ewe Nabii, «Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ya thawabu na neema yana manufaa zaidi kwenu kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Bora wa wanaoruzuku na kutoa, basi muombeni na mjisaidie kwa kumtii, ili myapate yaliyoko Kwake ya kheri mbili: ya duniani na ya Akhera. info
التفاسير: