ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
40 : 44

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ مِيقَٰتُهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Hakika Siku ya Uamuzi baina ya viumbe kwa waliyoyatanguliza katika dunia yao, ya kheri na ya shari, ndio wakati wa mkusanyiko wao wote. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 44

يَوۡمَ لَا يُغۡنِي مَوۡلًى عَن مَّوۡلٗى شَيۡـٔٗا وَلَا هُمۡ يُنصَرُونَ

Siku ambayo hakuna rafiki atayeweza kumuondolea rafiki yake shida yoyote, wala hawatasaidiana wao kwa wao, info
التفاسير:

external-link copy
42 : 44

إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemrehemu miongoni mwa Waumini, kwani yeye huenda akamuombea kwa Mola wake baada ya kuruhusiwa na Mwenyezi Mungu. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Mshindi katika kuwatesa maadui zake, Ndiye Mwenye kuwarehemu kwa wingi wale wenye kumtegemea na kumtii. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 44

إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ

Hakika mti wa zaqqūm unatoka kwenye shina la moto wa Jaḥīm. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 44

طَعَامُ ٱلۡأَثِيمِ

Matunda yake ni chakula cha mwenye dhambi nyingi, na dhambi kubwa zaidi kuliko dhambi zote ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 44

كَٱلۡمُهۡلِ يَغۡلِي فِي ٱلۡبُطُونِ

Matunda ya mti wa zaqqūm ni kama madini yaliyoyeyushwa. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 44

كَغَلۡيِ ٱلۡحَمِيمِ

Yanachoma ndani ya matumbo ya washirikina kama vile maji yaliyofikia upeo wa joto. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 44

خُذُوهُ فَٱعۡتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلۡجَحِيمِ

Mchukueni huyu mwenye dhambi aliyeasi mumsukume na mumuongoze kwa nguvu hadi katikati ya moto wa Jaḥīm Siku ya Kiyama. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 44

ثُمَّ صُبُّواْ فَوۡقَ رَأۡسِهِۦ مِنۡ عَذَابِ ٱلۡحَمِيمِ

Kisha mmimine juu ya kichwa cha huyu mfanya dhambi maji yaliyo moto sana hadi ya mwisho, na adhabu isimuepuke. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 44

ذُقۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡكَرِيمُ

Ataambiwa mfanya dhambi huyo mbaya, «Onja adhabu hii unayoadhibiwa kwayo Leo! Hakika wewe ni mheshimiwa katika watu wako, ulio mtukufu kwao.» Katika haya kuna kumfanyia maskhara na kumlaumu. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 44

إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمۡتَرُونَ

Hakika adhabu hii mnayoadhibiwa kwayo Leo, ndiyo ile adhabu mliokuwa mna shaka nayo duniani na mkawa hamuiamini. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 44

إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٖ

Hakika ya wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo yake duniani, watakuwa na mahali pa kukaa, hali ya kuwa wameaminika na magonjwa, masikitiko na mengineyo. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 44

فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ

Kwenye mabustani ya Pepo.na maji yenye kupita. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 44

يَلۡبَسُونَ مِن سُندُسٖ وَإِسۡتَبۡرَقٖ مُّتَقَٰبِلِينَ

Watakuwa wamevaa dibaji nyororo, hali ya kuwa wameelekeana kwa nyuso. Na hawatakuwa wakiangaliana visogo. Makao yao yatakuwa yakizunguka nao pale wanapozunguka. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 44

كَذَٰلِكَ وَزَوَّجۡنَٰهُم بِحُورٍ عِينٖ

Kama tutakavyowapa huko Akhera takrima ya kuwaingiza Peponi na kuwavisha hariri nzito na hariri yenye mng’aro, vilevile tutawakirimu kwa kuwaoza wanawake wazuri wenye macho makubwa ya kupendeza. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 44

يَدۡعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ

Wataka wachamungu hao huko Peponi waletewe kila aina ya matunda ya Peponi wanayoyatamani, wakiwa wamejiaminisha kuwa neema hizo hazitakatika wala hazitamalizika. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 44

لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلۡمَوۡتَ إِلَّا ٱلۡمَوۡتَةَ ٱلۡأُولَىٰۖ وَوَقَىٰهُمۡ عَذَابَ ٱلۡجَحِيمِ

Hawataonja kifo, wachamungu hao, huko Peponi, baada ya kifo cha kwanza walichokionja duniani. Na Mwenyezi Mungu Atawakinga , hao wachamungu,na adhabu ya moto wa Jaḥīm, kwa wema Wake na hisani itokayo Kwake, Aliyetakasika na kuwa juu. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 44

فَضۡلٗا مِّن رَّبِّكَۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Takrima hii tutakayowapa wachamungu, huko Akhera, ndiyo kufuzu kukubwa ambako hakuna kufuzu kungine baada ya kufuzu huko. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 44

فَإِنَّمَا يَسَّرۡنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمۡ يَتَذَكَّرُونَ

Hakika sisi tumeyarahisisha matamshi ya Qur’ani na maana yake kwa lugha yao, ewe Mtume, kwani huenda wakawaidhika na wakakemeeka. info
التفاسير:

external-link copy
59 : 44

فَٱرۡتَقِبۡ إِنَّهُم مُّرۡتَقِبُونَ

Basi ngojea, ewe Mtume, ushindi niliokuahidi juu ya hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu na adhabu itakayowashukia. Wao ni wenye kungojea kufa kwako, kukushinda na kukulazimisha. Basi watajua utakuwa ni wa nani ushindi, kufaulu na sauti ya juu duniani na Akhera. Hivyo ni vyako wewe, ewe Mtume, na vya wale Waumini waliokufuata. info
التفاسير: