ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
11 : 43

وَٱلَّذِي نَزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٖ فَأَنشَرۡنَا بِهِۦ بَلۡدَةٗ مَّيۡتٗاۚ كَذَٰلِكَ تُخۡرَجُونَ

Na Aliyeteremsha kutoka mawinguni mvua kwa kipimo, Asiifanye mafuriko yenye kuzamisha wala pungufu isiyotosheleza haja, ipate kuendesha maisha yenu na yale ya wanyama wenu, tukahuisha kwa maji hayo sehemu kubwa ya ardhi kavu isiyokuwa na mimea. Na kama tulivyotoa kwa maji hayo tuliyoyateremsha kutoka juu, kwenye ardhi hiyo iliyokufa, mimea na mazao, hivo ndivyo mtakavyotolewa, enyi watu, makaburini mwenu baada ya kutoweka kwenu. info
التفاسير:

external-link copy
12 : 43

وَٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡأَزۡوَٰجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡفُلۡكِ وَٱلۡأَنۡعَٰمِ مَا تَرۡكَبُونَ

Na Aliyeumba aina zote za wanyama na mimea, na Akawawekea majahazi mnayoyapanda baharini, na Akawaumbia wale mnaowapanda barani miongoni mwa wanyama, kama vile ngamia, farasi, nyumbu na punda. info
التفاسير:

external-link copy
13 : 43

لِتَسۡتَوُۥاْ عَلَىٰ ظُهُورِهِۦ ثُمَّ تَذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ رَبِّكُمۡ إِذَا ٱسۡتَوَيۡتُمۡ عَلَيۡهِ وَتَقُولُواْ سُبۡحَٰنَ ٱلَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُۥ مُقۡرِنِينَ

Mpate kujituliza juu ya migongo ya hivyo mnavyovipanda, kisha mkumbuke neema ya Mola wenu kwenu hapo mnapopanda na mseme, «Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Aliyetudhalilishia (kipando) hiki, na hatukuwa ni wenye uwezo juu yake.» info
التفاسير:

external-link copy
14 : 43

وَإِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ

Na ili mseme pia, «Na sisi baada ya kufa kwetu ni wenye kuelekea Kwake na kurejea. Hapa pana dalili ya kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kuwaneemesha waja Wake kwa neema mbalimbali, Ndiye Mwenye kustahiki kuabudiwa kwa kila hali. info
التفاسير:

external-link copy
15 : 43

وَجَعَلُواْ لَهُۥ مِنۡ عِبَادِهِۦ جُزۡءًاۚ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَكَفُورٞ مُّبِينٌ

Na hawa washirikina wamemfanya Mwenyezi Mungu kuwa na fungu miongoni mwa waja Wake. Nako ni kule kusema kwao kuhusu Malaika kuwa ni watoto wa kike wa mwenyezi Mungu. Kwa hakika, binadamu ni mwingi wa kukanusha neema za Mola Wake Alizowaneemesha kwazo, ni mwenye kudhihirisha kukataa kwake na kukanusha kwake, anahesabu misiba na anasahau neema. info
التفاسير:

external-link copy
16 : 43

أَمِ ٱتَّخَذَ مِمَّا يَخۡلُقُ بَنَاتٖ وَأَصۡفَىٰكُم بِٱلۡبَنِينَ

Je, kwani nyinyi mnadai, enyi wajinga, kuwa Mola wenu Amejichagulia, katika vile Anavyoviumba, watoto wa kike, na hali nyinyi hamliridhii hilo kwenu, na Akawahusu nyinyi kwa kuwapatia watoto wa kiume? Haya ni makaripio kwao. info
التفاسير:

external-link copy
17 : 43

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحۡمَٰنِ مَثَلٗا ظَلَّ وَجۡهُهُۥ مُسۡوَدّٗا وَهُوَ كَظِيمٌ

Na anapopewa bishara mmoja wao ya mtoto wa kike ambaye amemnasibishia Mwingi wa rehema, alipodai kwamba Malaika ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu, uso wake unageuka ukawa mweusi kwa bishara mbaya aliyopewa ya mtoto wa kike, na huwa na huzuni na kujawa na hamu na unguliko.(Basi vipi wataridhika kwa Mwenyezi Mungu kitu ambacho wao wenyewe hawaridhiki nacho? Ametukuka Mwenyezi Mungu kutukuka kukubwa na Ametakasika na kile wanachosema hao makafiri.) info
التفاسير:

external-link copy
18 : 43

أَوَمَن يُنَشَّؤُاْ فِي ٱلۡحِلۡيَةِ وَهُوَ فِي ٱلۡخِصَامِ غَيۡرُ مُبِينٖ

Je, mnajasiri na kumnasibishia Mwenyezi Mungu mtu anayelelewa katika pambo asiyeweza kutasua hoja kwenye mjadala kwa sababu ya kukulia kwake kwenye pambo na starehe? info
التفاسير:

external-link copy
19 : 43

وَجَعَلُواْ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ ٱلَّذِينَ هُمۡ عِبَٰدُ ٱلرَّحۡمَٰنِ إِنَٰثًاۚ أَشَهِدُواْ خَلۡقَهُمۡۚ سَتُكۡتَبُ شَهَٰدَتُهُمۡ وَيُسۡـَٔلُونَ

Na hawa washirikina waliwafanya Malaika ambao ni waja wa Mwenyezi Mungu kuwa ni wanawake. Je, wao walihudhuria wakati Mwenyezi Mungu Alipowaumba mpaka waamue kuwa wao ni wanawake? Ushahidi wao utasajiliwa, na wataulizwa kuhusu hilo kesho Akhera. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 43

وَقَالُواْ لَوۡ شَآءَ ٱلرَّحۡمَٰنُ مَا عَبَدۡنَٰهُمۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِنۡ هُمۡ إِلَّا يَخۡرُصُونَ

Na hawa washirikina wa Kikureshi wanasema, «Lau Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Angalitaka, hatungalimuabudu yoyote asiyekuwa Yeye.” Na hii ni hoja iliyotanguka, kwani Mwenyezi Mungu Ashasimamisha hoja juu ya waja kwa kuwatumiliza Mitume na kuteremsha Vitabu, basi kujisimamishia hoja ya Mapitisho na Makadirio ni ubatilifu mkubwa zaidi baada ya Mitume kuwaonya. Wao hawana ujuzi wa hakika ya yale wanayoyasema. Hakika ni kwamba wao wanayasema kwa kudhania na kuzua urongo, kwa kuwa hawana habari wala dalili kuhusu hilo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 43

أَمۡ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ كِتَٰبٗا مِّن قَبۡلِهِۦ فَهُم بِهِۦ مُسۡتَمۡسِكُونَ

Je, walishuhudia uumbaji wa Malaika au tuliwapatia kitabu kabla ya hii Qur’ani tuliyoiteremsha, wakawa wameshikamana nacho, wakifanyia kazi na wanajijengea kwa hicho hoja za kukupinga, ewe Mtume? info
التفاسير:

external-link copy
22 : 43

بَلۡ قَالُوٓاْ إِنَّا وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا عَلَىٰٓ أُمَّةٖ وَإِنَّا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم مُّهۡتَدُونَ

Bali walisema, «Sisi tuliwakuta baba zetu kwenye njia, madhehebu na dini, na sisi tunafuata na kuandama nyayo za baba zetu katika yale waliyokuwa nayo.” info
التفاسير: