ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
50 : 40

قَالُوٓاْ أَوَلَمۡ تَكُ تَأۡتِيكُمۡ رُسُلُكُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِۖ قَالُواْ بَلَىٰۚ قَالُواْ فَٱدۡعُواْۗ وَمَا دُعَٰٓؤُاْ ٱلۡكَٰفِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَٰلٍ

Washika hazina wa Jahanamu waseme kuwaambia kwa njia ya kuwakaripia na kuwalaumu, «Maombi haya hayatafalia kitu. Kwani hawakuwajia nyinyi Mitume wenu na hoja waziwazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na mkawakanusha?» Hapo wale wakanushaji walikubali hilo na wasema, «Ndio, wametujia.» Na washika hazina wa Jahanamu wajiepushe na wao na waseme, «Sisi hatutawaombea wala kuingilia kati kuhusu nyinyi. Ombeni nyinyi wenyewe, lakini dua hiyo haitafalia kitu, kwa kuwa nyinyi ni makafiri, na hayawi maombi ya makafiri isipokuwa ni yenye kupotea, hayakubaliwi wala hayaitikiwi.» info
التفاسير:

external-link copy
51 : 40

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَيَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ

Sisi tutawapa ushindi mitume wetu na wale waliowafuata, na tutawapa nguvu juu ya wale waliowaudhi katika uhai wa kilimwengu na Siku ya Kiyama, Siku ambayo watatoa ushahdi Malaika, Manabii na Waumini juu ya watu waliopita waliowakanusha Mitume wao; watatoa ushahidi kwamba Mitume walifikisha jumbe za Mola wao na kwamba watu hao waliwakanusha. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 40

يَوۡمَ لَا يَنفَعُ ٱلظَّٰلِمِينَ مَعۡذِرَتُهُمۡۖ وَلَهُمُ ٱللَّعۡنَةُ وَلَهُمۡ سُوٓءُ ٱلدَّارِ

Siku ya kuhesabiwa, hawatanufaika makafiri waliokiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu kwa zile nyudhuru wanazozitoa za kuwakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu. Watakalolipata ni kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, na watakuwa na Nyumba mbaya huko Akhera, nayo ni Moto. info
التفاسير:

external-link copy
53 : 40

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡهُدَىٰ وَأَوۡرَثۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡكِتَٰبَ

Kwa hakika tulimpa Mūsā Taurati na miujiza miongoni mwa vitu vinavyoongoza kwenye haki, na tukawafanya Wana wa Isrāīl warithiane Taurati: wanyuma kutoka kwa waliopita, info
التفاسير:

external-link copy
54 : 40

هُدٗى وَذِكۡرَىٰ لِأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِ

hali ya kuwa ni yenye kuongoza kwenye njia ya usawa na ni waadhi kwa wenye akili kamilifu. info
التفاسير:

external-link copy
55 : 40

فَٱصۡبِرۡ إِنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٞ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ بِٱلۡعَشِيِّ وَٱلۡإِبۡكَٰرِ

Basi subiri, ewe Mtume, juu ya udhia wa washirikina, kwani tumekuahidi kulitukuza neno lako, na ahadi yetu ni kweli haiendi kinyume, na utake msamaha wa dhambi zako, na uendelee daima kumtakasa Mola wako na kila sifa isiyonasibiana na Yeye katika kipindi cha mwisho wa mchana na mwanzo wake. info
التفاسير:

external-link copy
56 : 40

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِيٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيۡرِ سُلۡطَٰنٍ أَتَىٰهُمۡ إِن فِي صُدُورِهِمۡ إِلَّا كِبۡرٞ مَّا هُم بِبَٰلِغِيهِۚ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ

Hakika ya wale wanaoipinga haki kwa ubatilifu, na wanaozirudisha hoja sahihi kwa udanganyifu wa uharibifu bila ya kuwa na dalili wala ushahidi wala hoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, basi hamna ndani ya nyoyo za hao isipokuwa kuifanyia kiburi haki, kwa uhasidi wao juu ya fadhila ambazo Mwenyezi Mungu Amempa mtume Wake na utukufu wa utume ambao Amemkirimu nao, nayo ni mambo wao si wenye kuyafikia wala kuyapata. Basi shikamana na Mwenyezi Mungu akuhifadhi na shari lao, kwani Yeye ni Mwenye kuyasikia maneno yao , ni Mwenye kuyaona matendo yao, na Atawalipa kwayo. info
التفاسير:

external-link copy
57 : 40

لَخَلۡقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ أَكۡبَرُ مِنۡ خَلۡقِ ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ

Hakika ni kwamba uumbaji wa Mwenyezi Mungu wa mbingu na ardhi ni mkubwa zaidi kuliko kuwaumba watu na kuwarudisha uhai baada ya kufa, lakini wengi wa watu hawajui kwamba uumbaji wa vyote hivyo ni jambo sahali kwa Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
58 : 40

وَمَا يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَلَا ٱلۡمُسِيٓءُۚ قَلِيلٗا مَّا تَتَذَكَّرُونَ

Na halingani kipofu na anayeona, pia hawalingani Waumini wanaokubali kuwa Mwenyezi Mungu Ndiye Mungu wa haki Asiye na mshirika, wanaowaitikia Mitume Wake na wanaozifuata kivitendo Sheria Zake (hawalingani) na wenye kukataa ambao wanapinga kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki, na wakawakanusha Mitume Wake na wasizifuate Sheria Zake kivitendo. Ni uchache sana kwa nyinyi, enyi watu, kuzikumbuka hoja za Mwenyezi Mungu, mkazingatia na mkawaidhika nazo. info
التفاسير: