ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
84 : 38

قَالَ فَٱلۡحَقُّ وَٱلۡحَقَّ أَقُولُ

Mwenyezi Mungu Akasema, «Ukweli watoka kwangu , na sisemi isipokuwa ukweli. info
التفاسير:

external-link copy
85 : 38

لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ أَجۡمَعِينَ

Nitaujaza moto wa Jahanamu ukukusanye wewe na kizazi chako na wale wote wenye kukufuata miongoni mwa wanadamu.» info
التفاسير:

external-link copy
86 : 38

قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٖ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلۡمُتَكَلِّفِينَ

Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina miongoni mwa watu wako. «Sitaki kwenu ujira au malipo kwa kuwalingania nyinyi na kuwaongoza, na sidai jambo ambalo si langu, bali mimi nafuata yale ninayoletewa kwa njia ya wahyi, wala sijikalifishi kuleta mambo ya dhana na uzushi.» info
التفاسير:

external-link copy
87 : 38

إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٞ لِّلۡعَٰلَمِينَ

Haikuwa hii Qur’ani isipokuwa ni ukumbusho kwa viumbe vyote: majini na binadamu, wapate kujikumbusha kwayo mambo yanayowanufaisha wao ya maslahi ya Dini yao na dunia yao. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 38

وَلَتَعۡلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعۡدَ حِينِۭ

Na mtajua, tena mtajua, enyi washirikina, habari ya hii Qur’ani na ukweli wake, pindi utakaposhinda Uislamu na watu kuingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu mapote kwa mapote, na pia pindi mtakaposhukiwa na adhabu na kamba zote kuwakatikia. info
التفاسير: