ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
154 : 37

مَا لَكُمۡ كَيۡفَ تَحۡكُمُونَ

Ni uamuzi mbaya sana mnaoutoa, enyi watu, wa kuwa Mwenyezi Mungu Ana watoto wa kike na nyinyi mna watoto wa kiume, na hali nyinyi hamridhiki nafsi zenu kuwa na watoto wa kike. info
التفاسير:

external-link copy
155 : 37

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Je, hamkumbuki kwamba haifai wala haitakikani Awe na mtoto? Ametukuka Mwenyezi Mungu na kuwa mbali na hilo, umbali ulio juu sana. info
التفاسير:

external-link copy
156 : 37

أَمۡ لَكُمۡ سُلۡطَٰنٞ مُّبِينٞ

Lakini je, mna hoja ya wazi juu ya hilo neno lenu na uzushi wenu? info
التفاسير:

external-link copy
157 : 37

فَأۡتُواْ بِكِتَٰبِكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Iwapo mna hoja ndani ya kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu, basi kileteni, mkiwa ni wa kweli katika hilo neno lenu. info
التفاسير:

external-link copy
158 : 37

وَجَعَلُواْ بَيۡنَهُۥ وَبَيۡنَ ٱلۡجِنَّةِ نَسَبٗاۚ وَلَقَدۡ عَلِمَتِ ٱلۡجِنَّةُ إِنَّهُمۡ لَمُحۡضَرُونَ

Na washirikina walifanya kuwa kuna uhusiano wa kizazi baina ya Mwenyezi Mungu na Malaika, na hakika ni kwamba Malaika washajua kuwa washirikina ni wenye kuletwa Siku ya Kiyama ili kuadhibiwa. info
التفاسير:

external-link copy
159 : 37

سُبۡحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Ametakasika Mwenyezi Mungu na kila lisilofaa asifike nalo miongoni mwa yale wanaomsifu nayo washirikina. info
التفاسير:

external-link copy
160 : 37

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

Lakini wale waja wa Mwenyezi Mungu wanaomtakasia katika kumuabudu hawamsifu isipokuwa kwa sifa zinazolingana na utukufu Wake, kutakasika ni Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
161 : 37

فَإِنَّكُمۡ وَمَا تَعۡبُدُونَ

Hakika yenu nyinyi, enyi wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kile mnachokiabudu badala ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa waungu, info
التفاسير:

external-link copy
162 : 37

مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ بِفَٰتِنِينَ

hamkuwa ni wenye kumpoteza yoyote info
التفاسير:

external-link copy
163 : 37

إِلَّا مَنۡ هُوَ صَالِ ٱلۡجَحِيمِ

isipokuwa yule Aliyemkadiria Mwenyezi Mungu aingie kwenye Moto wa Jaḥīm kwa sababu ya ukafiri wake na udhalimu wake. info
التفاسير:

external-link copy
164 : 37

وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٞ مَّعۡلُومٞ

Malaika wanasema, «Hakuna yoyote miongoni mwetu isipokuwa ana makao maalumu mbinguni. info
التفاسير:

external-link copy
165 : 37

وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلصَّآفُّونَ

Na sisi ndio tunaosimama kwa kujipanga kwa safu katika kumuabudu Mwenyezi Mungu na kumtii. info
التفاسير:

external-link copy
166 : 37

وَإِنَّا لَنَحۡنُ ٱلۡمُسَبِّحُونَ

Na sisi ndio tunaomtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisichofaa kunasibishwa nacho.» info
التفاسير:

external-link copy
167 : 37

وَإِن كَانُواْ لَيَقُولُونَ

Na hakika makafiri wa Makkah walikuwa wakisema kabla hujatumilizwa, info
التفاسير:

external-link copy
168 : 37

لَوۡ أَنَّ عِندَنَا ذِكۡرٗا مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ

«Ewe Mtume! Lau vingalitujia vitabu na Manabii vile vilivyowajia wa mwanzo kabla yetu, info
التفاسير:

external-link copy
169 : 37

لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلۡمُخۡلَصِينَ

tungalikuwa waja wa Mwenyezi Mungu wakweli katika Imani, waliotakaswa kwa kufanya Ibada.» info
التفاسير:

external-link copy
170 : 37

فَكَفَرُواْ بِهِۦۖ فَسَوۡفَ يَعۡلَمُونَ

Ulipowajia wao utajo wa watu wa mwanzo na utajo wa watu wa mwisho na kitabu kikamilifu kabisa na bora wa Mitume, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, walimkanusha. Basi wataijua adhabu watakayopatiwa Siku ya Mwisho. info
التفاسير:

external-link copy
171 : 37

وَلَقَدۡ سَبَقَتۡ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Kwa hakika lishatangulia neno letu, ambalo halina namna ya kurudi, la kuwaahidi waja wetu waliopewa utume info
التفاسير:

external-link copy
172 : 37

إِنَّهُمۡ لَهُمُ ٱلۡمَنصُورُونَ

kwamba watapata usaidizi juu ya maadui zao, kwa hoja na nguvu, info
التفاسير:

external-link copy
173 : 37

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلۡغَٰلِبُونَ

na kwamba askari wetu wanaopigana jihadi katika njia yetu ndio wenye kuwashinda maadui zao kila mahali, kuzingatia mwishoni na marejeo. info
التفاسير:

external-link copy
174 : 37

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ

Basi wape mgongo, ewe Mtume, wale walioshindana na wasiikubali haki mpaka ukamalizika muda waliopatiwa muhula na ikaja amri ya Mwenyezi Mungu ya wao kuadhibiwa, info
التفاسير:

external-link copy
175 : 37

وَأَبۡصِرۡهُمۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ

wangojee na subiri uone: ni adhabu gani itakayowashukia wao kwa kuenda kinyume nawe? Basi wataiona adhabu ya Mwenyezi Mungu itakayowashukia. info
التفاسير:

external-link copy
176 : 37

أَفَبِعَذَابِنَا يَسۡتَعۡجِلُونَ

Je kuteremkiwa kwao na adhabu yetu ndilo jambo wanalokuharakishia, ewe Mtume? info
التفاسير:

external-link copy
177 : 37

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمۡ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلۡمُنذَرِينَ

Basi adhabu yetu itakapowashukia, asubuhi mbaya zaidi ni asubuhi yao! info
التفاسير:

external-link copy
178 : 37

وَتَوَلَّ عَنۡهُمۡ حَتَّىٰ حِينٖ

Na uwape mgongo mpaka Mwenyezi Mungu Atoe idhini ya wao kuadhibiwa. info
التفاسير:

external-link copy
179 : 37

وَأَبۡصِرۡ فَسَوۡفَ يُبۡصِرُونَ

Na uwangojee, kwani wataiona adhabu itakayowashukia na mateso. info
التفاسير:

external-link copy
180 : 37

سُبۡحَٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلۡعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ

Mola wa enzi na utukufu Ameepukana na kuwa juu ya kila kile ambacho wanaomzulia urongo wanamsifu nacho. info
التفاسير:

external-link copy
181 : 37

وَسَلَٰمٌ عَلَى ٱلۡمُرۡسَلِينَ

Na maamkizi ya Mwenyezi Mungu ya daima,sifa Zake na amani Yake ziwafikie Mitume wote. info
التفاسير:

external-link copy
182 : 37

وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Na shukrani na sifa njema ni za Mola wa viumbe wote ulimwenguni na Akhera. Yeye Ndiye Mstahiki wa hilo Peke Yake, Hana mshirika Wake. info
التفاسير: