ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

external-link copy
46 : 3

وَيُكَلِّمُ ٱلنَّاسَ فِي ٱلۡمَهۡدِ وَكَهۡلٗا وَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Na atasema na watu na hali yeye ni mtoto mchanga wa kunyonya kabla hajafikia wakati wa kusema. Na atawaita wao kwa Mwenyezi Mungu, akiwa mkubwa wakati ambapo nguvu zake zitakuwa zimeshikana na ubarobaro wake umekamilika, kwa yale aliyoletewa wahyi na Mwenyezi Mungu. Kusema huku ni kuhusu utume, ulinganizi na uongozi. Na yeye anahesabiwa kuwa ni mmoja wa watu wema na wenye utukufu wa maneno na vitendo. info
التفاسير: