ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

external-link copy
168 : 3

ٱلَّذِينَ قَالُواْ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ وَقَعَدُواْ لَوۡ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُواْۗ قُلۡ فَٱدۡرَءُواْ عَنۡ أَنفُسِكُمُ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Wanafiki hawa ndio wale walioketi wakawaambia ndugu zao waliopata msiba pamoja na Waislamu kwenye vita vyao na washirikina siku ya Uhud, «Lau kama watu hawa wangalitutii hawangaliuawa.» Sema, ewe Mtume, uwaambie «Zizuieni nafsi zenu na kifo, ikiwa nyinyi ni wa kweli katika madai yenu kwamba wao kama wangaliwatii hawangaliuawa na kwamba mumeokoka na mauti kwa kukaa kwenu kutokwenda vitani.» info
التفاسير: