ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាswahili - អាប់ឌុលឡោះ ម៉ូហាំម៉ាត់ និងណាសៀរ ខមុីស

external-link copy
105 : 17

وَبِٱلۡحَقِّ أَنزَلۡنَٰهُ وَبِٱلۡحَقِّ نَزَلَۗ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Na tumemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, hii Qur’ani ili kuwaamrisha waja, kuwakataza, kuwalipa mema na kuwaadhibu; na imeteremka kwa ukweli, uadilifu na utunzi isibadilishwe na isigeuzwe. Na hatukukutumiliza wewe, ewe Mtume, isipokuwa ni uwabashirie Pepo waliotii na uwatishe na Moto walioasi na kukanusha. info
التفاسير: