Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani

external-link copy
81 : 28

فَخَسَفۡنَا بِهِۦ وَبِدَارِهِ ٱلۡأَرۡضَ فَمَا كَانَ لَهُۥ مِن فِئَةٖ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلۡمُنتَصِرِينَ

Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanao jitetea. [81] info

[81] Mwenyezi Mungu akamdidimiza katika ardhi, na ardhi ikammeza yeye na nyumba yake na vyote vilio kuwemo ndani yake, mali na mapambo yake. Hakuwa na wasaidizi wa kumkinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na wala yeye mwenyewe hakuweza kujinusuru nafsi yake.

التفاسير: