Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani

external-link copy
31 : 28

وَأَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۚ فَلَمَّا رَءَاهَا تَهۡتَزُّ كَأَنَّهَا جَآنّٞ وَلَّىٰ مُدۡبِرٗا وَلَمۡ يُعَقِّبۡۚ يَٰمُوسَىٰٓ أَقۡبِلۡ وَلَا تَخَفۡۖ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡأٓمِنِينَ

Na tupa chini fimbo yako. Basi alipo iona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma wala hakutazama. (Akaambiwa): Ewe Musa! Njoo mbele wala usiogope. Hakika wewe ni miongoni mwa walio salimika. info

Na akanadiwa: Tupa chini fimbo yako. Akaitupa chini. Mwenyezi Mungu akaigeuza ikawa nyoka. Musa alipo iona inakwenda kama nyoka alikhofu, na akakimbia kwa kufazaika. Akaambiwa: Ewe Musa! Njoo, unaitwa urejee pahala pako, wala usiogope. Kwani wewe ni katika walio hifadhiwa na kila cha kuchukiza.

التفاسير: