Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani

external-link copy
29 : 28

۞ فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى ٱلۡأَجَلَ وَسَارَ بِأَهۡلِهِۦٓ ءَانَسَ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ نَارٗاۖ قَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِخَبَرٍ أَوۡ جَذۡوَةٖ مِّنَ ٱلنَّارِ لَعَلَّكُمۡ تَصۡطَلُونَ

Basi alipo timiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa Mlima T'uri. Akawaambia ahali zake: Ngojeni! Mimi nimeona moto, labda nitakuleteeni kutoka huko khabari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto. info

Musa alipo timiza muda wake walio patana, na akawa mume wa binti wa yule aliye mpokea, na akawa anarudi Misri, aliona njiani mwake katika upande wa Mlima wa T'uri moto unawaka. Akawaambia walio kuwa pamoja naye: Kaeni hapa. Mimi nimeuona moto, nimefurahi nao katika giza hili. Nitawendea nikuleteeni khabari ya njia, au nipate kijinga cha moto mpate walau moto wa kuota kujilinda na baridi.

التفاسير: