[91] Pamoja na hawa simulia kisa cha Maryamu aliye ulinda uke wake, nasi tukamfikishia siri katika siri zetu. Tukamjaalia achukue mimba bila ya mume, na tukamjaalia mwanawe azaliwe bila ya baba. Akawa yeye na mwanawe dalili iliyo wazi ya uweza wetu kugeuza sababu na vinavyo sabibishwa. Na hakika Sisi ni waweza wa kila kitu.