Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
36 : 69

وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنۡ غِسۡلِينٖ

wala hatakuwa na chakula isipokuwa kile kinachotokana na usaa wa watu wa motoni, info
التفاسير:

external-link copy
37 : 69

لَّا يَأۡكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلۡخَٰطِـُٔونَ

hakuna mwenye kukila isipokuwa wale wenye dhambi, wanaoshikilia kumkanusha Mwenyezi mungu. info
التفاسير:

external-link copy
38 : 69

فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَا تُبۡصِرُونَ

Naapa kwa mnavyoviona miongoni mwa vitu vinavyooonekana, info
التفاسير:

external-link copy
39 : 69

وَمَا لَا تُبۡصِرُونَ

na vile msivyoviona miongoni mwa vile vilivyoghibu kwenu., hakika Qur’ani ni maneno ya Mwenyezi Mungu. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 69

إِنَّهُۥ لَقَوۡلُ رَسُولٖ كَرِيمٖ

Inasomwa na mjumbe mkubwa wa cheo na utukufu. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 69

وَمَا هُوَ بِقَوۡلِ شَاعِرٖۚ قَلِيلٗا مَّا تُؤۡمِنُونَ

Na si maneno ya mshairi kama mnavyodai, ni uchache mno mnavyoamini. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 69

وَلَا بِقَوۡلِ كَاهِنٖۚ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ

Wala si tungo kama zile tungo za makuhani, ni kuchache mno kule kukumbuka kwenu na kutia akilini kuwa kuna tafauti baina ya mawili hayo. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 69

تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Lakini hiyo Qur’ani ni maneno ya Mola wa viumbe wote Aliyoyateremshia Mtume Wake Muhaammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info
التفاسير:

external-link copy
44 : 69

وَلَوۡ تَقَوَّلَ عَلَيۡنَا بَعۡضَ ٱلۡأَقَاوِيلِ

Na lau Muhammad angalitusingizia maneno tusiyoyanena info
التفاسير:

external-link copy
45 : 69

لَأَخَذۡنَا مِنۡهُ بِٱلۡيَمِينِ

tungalimtesa na tungalimkamata kwa nguvu na uweza, kwani nguvu ya kila kitu iko kwenye upande wake wa kulia, info
التفاسير:

external-link copy
46 : 69

ثُمَّ لَقَطَعۡنَا مِنۡهُ ٱلۡوَتِينَ

kisha tungalimkata mshipa wa moyo wake., info
التفاسير:

external-link copy
47 : 69

فَمَا مِنكُم مِّنۡ أَحَدٍ عَنۡهُ حَٰجِزِينَ

hataweza yoyote kuyazuia mateso yetu yasimpate. info
التفاسير:

external-link copy
48 : 69

وَإِنَّهُۥ لَتَذۡكِرَةٞ لِّلۡمُتَّقِينَ

Na hii Qur’ani ni mawaidha kwa wachamungu wanaofuata amri za Mwenyezi Mungu na kuyaepuka makatazo yake. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 69

وَإِنَّا لَنَعۡلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ

Na sisi kwa hakika tunajua kwamba miongoni mwenu kuna wanaoikanusha hii Qur’ani pamoja na kuwa dalili zake ziko wazi. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَسۡرَةٌ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na kwa hakika kuikanusha Qur’ani ni majuto makubwa kwa wenye kuikanusha pindi watakapoiona adhabu yao na kuona starehe za wenye kuiamini. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 69

وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلۡيَقِينِ

Na kwa hakika hii Qur’ani ni haki iliyothibiti na yakini isiyo na shaka. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 69

فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ

Basi Mwepushie Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kila sifa isiyonasibiana na haiba Yake, na umtaje kwa jina Lake tukufu. info
التفاسير: