Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

As-Saff

external-link copy
1 : 61

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vimemtakasa Mwenyezi Mungu na kumwepusha na kila kisichonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na Yeye ni Mshindi Ambaye hakuna mwenye kushindana na Yeye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. info
التفاسير: