Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

external-link copy
112 : 5

إِذۡ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ يَٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ هَلۡ يَسۡتَطِيعُ رَبُّكَ أَن يُنَزِّلَ عَلَيۡنَا مَآئِدَةٗ مِّنَ ٱلسَّمَآءِۖ قَالَ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na ukumbuke waliposema Ḥawāriyyūn (wasafiwa wa Nabii ‘Īsā kati ya wafuasi wake), «Ewe ‘Īsā mwana wa Maryam! Je, Anaweza Mola wako, ukimuomba, kututeremshia meza ya chakula kutoka mbinguni?» Jawabu yake ilikuwa ni kuwataka wao wajikinge na adhabu ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, wakiwa ni wenye kuamini Imani ya kikweli. info
التفاسير: