Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Al-Fath

external-link copy
1 : 48

إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحٗا مُّبِينٗا

Sisi tumekufungulia wewe, ewe Mtume, ufunguzi ulio waziwazi, ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Ataipa nguvu Dini Yako na Atakupa ushindi juu ya maadui wako, nao ni mapatano ya Ḥudaybiyah ambayo kwayo watu walikuwa katika hali ya amani, na likapanuka duara la ulinganizi wa Dini ya Mwenyezi Mungu, na watu wakaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu mapote kwa mapote. Kwa hivyo, Mwenyezi Mung Aliyaita mapatano hayo “Ufunguzi uliofunuka” yaani uliokuwa wazi wenye kujitokeza. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 48

لِّيَغۡفِرَ لَكَ ٱللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنۢبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعۡمَتَهُۥ عَلَيۡكَ وَيَهۡدِيَكَ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا

Tumekufungulia ufunguzi huo na tukakufanyia sahali, ili Mwenyezi Mungu Akusamehe dhambi zako zilizotangulia na zitakazofanyika baadaye, kwa sababu ya utiifu mwingi ulioufanya unaotokana na ufunguzi huu na kwa usumbufu ulioubeba, na ili Akutimizie neema Zake kwako kwa kuipa ushindi Dini yako, info
التفاسير:

external-link copy
3 : 48

وَيَنصُرَكَ ٱللَّهُ نَصۡرًا عَزِيزًا

Akunusuru juu ya maadui wako na Akuongoze njia ya Dini iliyolingana sawa isiyopotoka , na Mwenyezi Mugu Akunusuru kwa nguvu kwa namna ambayo Uislamu hautakuwa mnyonge. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 48

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِيمَٰنٗا مَّعَ إِيمَٰنِهِمۡۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا

Yeye Ndiye Mwenyezi Mungu Aliyeteremsha utulivu ndani ya nyoyo za wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake katika siku ya Ḥudaybiyah zikatulia na yakini ikajidhatititi ndani ya hizo nyoyo, ili wazidi kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake pamoja na kuamini kwao na kufuata kwao. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Ana askari wa mbinguni na ardhini, Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa maslahi ya viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na utengezaji Wake. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 48

لِّيُدۡخِلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِهِمۡۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِندَ ٱللَّهِ فَوۡزًا عَظِيمٗا

Apate kuwaingiza Waumini wa kiume na Waumini wa kike kwenye mabustani ya Peponi ambayo mito inapita chini ya miti yake na majumba yake ya fahari, hali ya kukaa humo milele, na Awafutie baya walilolifanya asiwaadhibu kwalo. Malipo hayo kwa Mwenyezi Mungu ndio kuokoka na kila kero na ndio kupata kila linalotafutwa. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 48

وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ ٱلظَّآنِّينَ بِٱللَّهِ ظَنَّ ٱلسَّوۡءِۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۖ وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَلَعَنَهُمۡ وَأَعَدَّ لَهُمۡ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرٗا

Na Apate kuwaadhibu wanafiki wa kiume na wanafiki wa kike na washirikina wa kiume na washirikina wa kike wanaomdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya ya kuwa yeye Hatamnusuru Mtume na waliokuwa pamoja na yeye dhidi ya maadui wao na kuwa Yeye Hataipa ushindi Dini Yake. Basi juu ya hao utazunguka mzunguko wa adhabu na kila kilicho kibaya kwao, na Amewaandalia moto wa Jahanamu; na mashukio mabaya ya mtu kuishia ni hayo. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 48

وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمًا

Na Mwenyezi Mungu, Alyetakasika na kutukuka, Ana askari wa mbinguni na ardhini. Anawanusuru kwa askari hao waja Wake Waumini. Na Mwenyezi Mungu ni Mshindi Mwenye uweza juu viumbe Vyake, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo yao. info
التفاسير:

external-link copy
8 : 48

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا

Hakika yetu sisi tumekutumiliza, ewe Mtume, uwe shahidi kwa umati wako juu ya ufikishaji ujumbe, uwabainishie kile ulichotumilizwa kwao, uwabashirie Pepo wanaokutii na uwaonye mateso ya sasa na ya baadaye, info
التفاسير:

external-link copy
9 : 48

لِّتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُعَزِّرُوهُ وَتُوَقِّرُوهُۚ وَتُسَبِّحُوهُ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلًا

mpate kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, mumnusuru Mwenyezi Mungu kwa kuinusuru Dini Yake, mumtukuze na mumtakase mwanzo wa mchana na mwisho wake. info
التفاسير: