Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

external-link copy
7 : 47

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن تَنصُرُواْ ٱللَّهَ يَنصُرۡكُمۡ وَيُثَبِّتۡ أَقۡدَامَكُمۡ

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mkiinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu kwa kupigana jihadi katika njia Yake na kuhukumu kwa Kitabu Chake na kufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake, Mwenyezi Mungu Atawapa ushindi juu ya maadui zenu na Atazithibitisha nyayo zenu wakati wa kupigana. info
التفاسير: