Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Ash-Shura

external-link copy
1 : 42

حمٓ

«Ḥā, Mīm, info
التفاسير:

external-link copy
2 : 42

عٓسٓقٓ

'Ayn, Sīn, Qāf» Yametangulia maelezo juu ya herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 42

كَذَٰلِكَ يُوحِيٓ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Kama Alivyokuteremshia Mwenyezi Mungu, ewe Nabii, hii Qur’ani, Aliteremsha Vitabu na Kurasa kwa Manabii kabla yako. Na Yeye Ndiye Mshindi katika kutesa Kwake, Ndiye Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 42

لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Ni vya Mwenyezi Mungu Peke Yake vilivyoko mbinguni na ardhini, na Yeye Ndiye wa juu kwa cheo Chake na utendeshaji nguvu Wake, Aliye Mkuu Ambaye Ana ukubwa na enzi. info
التفاسير:

external-link copy
5 : 42

تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِن فَوۡقِهِنَّۚ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Zinakaribia mbingu kupasuka- pasuka, kila moja juu ya ile inayoifuata, kutokana na ukubwa wa Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema na haiba Yake, Mwingi wa fadhila na utukufu, na hali Malaika wanamtakasia Shukurani Mola wao na kumwepusha na kila sifa ambayo hanasibiani nayo, na wanamuomba Mola wao msamaha wa dhambi za waliyoko ardhini miongoni mwa wale wanaomuamini. Jueni mtanabahi kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Mwenye kusamehe sana dhambi za waja Wake Waumini na Ndiye Mwenye kuwarehemu. info
التفاسير:

external-link copy
6 : 42

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيۡهِمۡ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٖ

Na wale waliowafanya wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni waungu badala Yake wakawategemea na kuwaabudu, basi Mwenyezi Mungu Anavidhibiti vitendo vyao, ili Awalipe kwavyo Siku ya Kiyama. Na wewe hukuwakilishwa kuvidhibiti vitendo vyao. Hakika yako wewe ni muonyaji tu, hivyo basi ni juu yako kufikisha na ni juu yetu kuhesabu. info
التفاسير:

external-link copy
7 : 42

وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَا وَتُنذِرَ يَوۡمَ ٱلۡجَمۡعِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ فَرِيقٞ فِي ٱلۡجَنَّةِ وَفَرِيقٞ فِي ٱلسَّعِيرِ

Na kama tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako wewe, tulikuletea wahyi wa Qur’ani iliyo kwa lugha ya Kiarabu, ili uwaonye watu wa Makkah na watu wote wengine pambizoni mwake[9], na uwaonye Siku ya Mkusanyiko, nayo ni Siku ya Kiyama, ambayo kuja kwake hakuna shaka, ambapo watu Siku hiyo watakuwa mapote mawili: pote moja litakuwa Peponi, nalo ni lile la waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakayafuata yale aliyokuja nayo Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na pote lingine litakuwa Motoni, nalo ni lile la waliomkanusha Mwenyezi Mungu na wakaenda kinyume na yale aliyokuja nayo Mtume Wake, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. info

[9]Kwa kuwa Makkah ni kituo cha ardhi Umm al Qurā (Mama wa miji) kwa kuwu ni mji mtukufu kuliko miji yote, ndio ikawa miji yote mingine pamoja na watu wake huwa imeizunguka Makkah na iko pambizoni mwake. Utukufu wa Makkah juu ya sehemu zote za ardhi pia umithibiti kwenye hadithi za Mtum (s.a.w). Ang. Tafsiri ya Ibn Kathīr katika kufasiri aya hii: 42 :7.

التفاسير:

external-link copy
8 : 42

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَهُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na lau Angalitaka Mwenyezi Mungu Kuwakusanya viumbe Wake kwenye uongofu na kuwafanya wawe kwenye mila moja iliyoongoka angalifanya hivyo, lakini Yeye Anataka kuwatia kwenye rehema Yake Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Na wale wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kufanya ushirikina, basi hao hawatakuwa na yoyote wa kumtegemea atakayesimamia mambo yao Siku ya Kiyama, wala msaidizi atakayewanusuru kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. info
التفاسير:

external-link copy
9 : 42

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۖ فَٱللَّهُ هُوَ ٱلۡوَلِيُّ وَهُوَ يُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Bali hawa washirikina waliwachukuwa wasiokuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni wategemewa wakawa wanawategemea. Mwenyezi Mungu Peke Yake Ndiye Mwenye kutegemewa, mja anamtegemea kwa kumuabudu na kumtii, na Yeye Anawasimamia waja Wake Waumini kwa kuwatoa kwenye giza kuwatia kwenye mwangaza na kwa kuwasaidia katika mambo yao yote. Na Yeye Anahuisha waliokufa wakati wa kufufuliwa, na Yeye kwa kila jambo ni Mweza, hakuna chochote kinachomshinda. info
التفاسير:

external-link copy
10 : 42

وَمَا ٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِيهِ مِن شَيۡءٖ فَحُكۡمُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبِّي عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ

Na kitu chochote kile mnachotafautiana kwacho , enyi watu, miongoni mwa mambo ya dini yenu, basi hukumu irudishwe kwa Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake na Sunnah ya Mtume Wake, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie. Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wangu na Mola wenu, Kwake Yeye nimetegemea katika mambo yangu, na Kwake Yeye ninarejea katika hali zangu zote. info
التفاسير: