Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
41 : 40

۞ وَيَٰقَوۡمِ مَا لِيٓ أَدۡعُوكُمۡ إِلَى ٱلنَّجَوٰةِ وَتَدۡعُونَنِيٓ إِلَى ٱلنَّارِ

«Na enyi watu wangu! Vipi mimi ninawalingania kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake Mūsā, nao ni ulinganizi utakaowafanya nyinyi muishie Peponi na muwe mbali na vituko vya Moto, na nyinyi mnanilingania kufany matendo yenye kupelekea kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso Yake Motoni.? info
التفاسير:

external-link copy
42 : 40

تَدۡعُونَنِي لِأَكۡفُرَ بِٱللَّهِ وَأُشۡرِكَ بِهِۦ مَا لَيۡسَ لِي بِهِۦ عِلۡمٞ وَأَنَا۠ أَدۡعُوكُمۡ إِلَى ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡغَفَّٰرِ

«Mnanilingania mimi nimkanushe Mwenyezi Mungu na nimshirikishe Yeye na kitu amabacho sina ujuzi nacho kuwa kinastahiki kuabudiwa badala Yake- na hili ni miongoni madhambi makubwa zaidi na maovu zaidi- Na mimi ninawalingania kwenye njia yenye kupelekea kwa Mwenyezi Mungu Aliye Mshindi katika kutesa Kwake, Mwingi wa msamaha kwa aliyerudia Kwake kwa kutubia baada ya kumuasi. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 40

لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدۡعُونَنِيٓ إِلَيۡهِ لَيۡسَ لَهُۥ دَعۡوَةٞ فِي ٱلدُّنۡيَا وَلَا فِي ٱلۡأٓخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَآ إِلَى ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ هُمۡ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ

«Ukweli ni kwamba kile mnachoniitia kukiamini hakistahiki kuitiwa wala kutegemewa kwa kupata himaya duniani wala Akhera kwa kuwa chenyewe kina udhaifu na upungufu. Na mjuwe kwamba mwisho wa viumbe vyote ni kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika, na Yeye Atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake, na wale waliokiuka mipaka Yake kwa kufanya vitendo vya uasi, kumwaga damu na kukanusha, wao ndio watu wa Motoni.» info
التفاسير:

external-link copy
44 : 40

فَسَتَذۡكُرُونَ مَآ أَقُولُ لَكُمۡۚ وَأُفَوِّضُ أَمۡرِيٓ إِلَى ٱللَّهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ بَصِيرُۢ بِٱلۡعِبَادِ

Alipowasihi na wasimkubalie aliwaambia, «Basi mtakumbuka kuwa mimi niliwasihi na nikawakumbusha, na mtajuta wakati ambao majuto hayatanufaisha. Na mimi ninahamia kwa Mola wangu nataka hifadhi Yake na ninamtegemea Yeye, hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, ni Mtambuzi wa hali za waja na malipo wanayostahiki malipo, hakuna kinachofichamana Kwake chochote katika hayo.» info
التفاسير:

external-link copy
45 : 40

فَوَقَىٰهُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِ مَا مَكَرُواْۖ وَحَاقَ بِـَٔالِ فِرۡعَوۡنَ سُوٓءُ ٱلۡعَذَابِ

Basi Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Akamuokoa mtu huyo aliyeamini na mateso ya vitimbi vya Fir’awn na jamaa zake, na ikawashukia wao adhabu mbaya, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliwazamisha wote mpaka wa mwisho wao. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 40

ٱلنَّارُ يُعۡرَضُونَ عَلَيۡهَا غُدُوّٗا وَعَشِيّٗاۚ وَيَوۡمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ أَدۡخِلُوٓاْ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ أَشَدَّ ٱلۡعَذَابِ

Kwanza walipatikana na gharika wakaangamia, kisha wakawa wanaadhibiwa ndani ya makaburi yao ambapo Moto unaorodheshwa kwao, asubuhi na jioni, mpaka wakati wa kuhesabiwa. Na Siku ambayo Kiyama kitasimama kutasemwa, «Watieni Motoni jamaa wa Fir’awn ukiwa ni malipo ya matendo mabaya waliyoyatenda.» Aya hii ndio msingi wa kuthibitisha adhabu ya kaburini. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 40

وَإِذۡ يَتَحَآجُّونَ فِي ٱلنَّارِ فَيَقُولُ ٱلضُّعَفَٰٓؤُاْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُنَّا لَكُمۡ تَبَعٗا فَهَلۡ أَنتُم مُّغۡنُونَ عَنَّا نَصِيبٗا مِّنَ ٱلنَّارِ

Na pindi watakapogombana watu wa Motoni na kulaumiana wao kwa wao, hapo wajenge hoja wafuasi wenye kuandama dhidi ya viongozi wao wenye kiburi ambao waliwapoteza na wakawapambia njia ya uovu, kwa kuwaambia, «Je, nyinyi mtatuondolea sehemu ya Moto kwa kujibebesha fungu la adhabu yetu?» info
التفاسير:

external-link copy
48 : 40

قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا كُلّٞ فِيهَآ إِنَّ ٱللَّهَ قَدۡ حَكَمَ بَيۡنَ ٱلۡعِبَادِ

Viongozi waliokuwa na kiburi watasema, wakieleza ulemevu wao, «Hatutawabebea kitu chochote cha adhabu ya Moto, na hali sisi sote tumo ndani yake, hatuna namna ya kuokoka nao, Mwenyezi Mungu Amegawanya adhabu baina yetu kwa uamuzi Wake wa haki, kila mmoja wetu kwa kadiri anayostahiki.» info
التفاسير:

external-link copy
49 : 40

وَقَالَ ٱلَّذِينَ فِي ٱلنَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ٱدۡعُواْ رَبَّكُمۡ يُخَفِّفۡ عَنَّا يَوۡمٗا مِّنَ ٱلۡعَذَابِ

Na watasema wale waliyomo Motoni miongoni mwa watu wakubwa wenye kiburi na wanyonge wakiwaambia walinzi wa Jahanamu, «Muombeni Mola wenu atusahilishie adhabu kwa siku moja ili tupate kiasi fulani cha mapumziko.» info
التفاسير: