Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
41 : 39

إِنَّآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ لِلنَّاسِ بِٱلۡحَقِّۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَلِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٍ

Hakika sisi tumekuteremshia wewe, ewe Mtume, Qur’ani kwa haki ikiwa ni yenye kuwaongoza viumbe wote kwenye njia ya uongofu. Basi mwenye kuongoka kwa mwangaza wake na akayatumia yaliyomo ndani yake na akasimama imara kufuata njia yake, basi manufaa ya kufanya hilo yatamrudia mwenyewe. Na mwenye kupotea baada ya kubainikiwa na uongofu, basi madhara yake yatamrudia mwenyewe, na hilo halitamdhuru Mwenyezi Mungu kitu chochote. Na hukuwa wewe, ewe Mtume, ni mwakilishwa wa kuyatunza matendo yao, kuwahesabu kwa hayo na kuwalazimisha unayoyataka, jukumu lako wewe si lingine isipokuwa ni kufikisha ujumbe. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 39

ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلۡأَنفُسَ حِينَ مَوۡتِهَا وَٱلَّتِي لَمۡ تَمُتۡ فِي مَنَامِهَاۖ فَيُمۡسِكُ ٱلَّتِي قَضَىٰ عَلَيۡهَا ٱلۡمَوۡتَ وَيُرۡسِلُ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Mwenyezi Mungu Ndiye Anayezikamata nafsi wakati zinapokufa. Kufa huku ni kufa kukubwa, kufa kwa kushukiwa na mauti kwa ajali kukoma. Na zile nafsi ambazo hazikufa Anazikamata katika hali ya kulala kwake, nako ndiko kufa kudogo. Hivyo basi Akazizuia, kati ya hizi nafsi mbili, ile Aliyoitolea uamuzi ife , nayo ni ya yule aliyekufa, na anaiachilia nafsi nyingine mpaka ikamilishe muda wake wa kuishi na riziki yake, nako ni kuirudisha kwenye mwili wa mwenye nafsi hiyo. Kwa kweli, katika kule kukamata kwa Mwenyezi Mungu nafsi ya aliyekufa na aliyelala na kuiachilia nafsi ya aliyelala na kuizuia nafsi ya aliyekufa kuna dalili waziwazi za uweza wa Mwenyezi Mungu kwa anayefikiria na kuzingatia. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 39

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُفَعَآءَۚ قُلۡ أَوَلَوۡ كَانُواْ لَا يَمۡلِكُونَ شَيۡـٔٗا وَلَا يَعۡقِلُونَ

Au kwani hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu wamewachukua badala Yake Yeye waungu wao wanaowaabudu wakawafanya ni waombezi wakuwaombea kwa Mwenyezi Mungu katika haja zao? Waambie, «Je mnawafanya ni waombezi kama mnavyodai, ingawa waungu hao hawamiliki chochote na hawafahamu kamwe kuwa nyinyi mnawaabudu? info
التفاسير:

external-link copy
44 : 39

قُل لِّلَّهِ ٱلشَّفَٰعَةُ جَمِيعٗاۖ لَّهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ ثُمَّ إِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Waambie, ewe Mtume, hao washirikina, «Ni wa Mwenyezi Mungu uombezi wote. Ni Yake Yeye mamalaka ya mbinguni na ardhini na vilivyoko baina yake. Amri yote ni ya Mwenyezi Mungu Peke Yake. Na hakuna yoyote atakayeombea mbele Yake isipokuwa kwa idhini Yake. Yeye Ndiye Anayemiliki mbingu na ardhi na anayeendesha mambo yake. Lilo wajibu ni kutakwa uombezi kutoka kwa anayeumiliki na atakasiwe Yeye kwa ibada, na usitakwe kutoka kwa waungu wasiodhuru wala kunufaisha, kisha Kwake Yeye mtarudishwa baada ya kufa kwenu ili mhesabiwe na mlipwe. info
التفاسير:

external-link copy
45 : 39

وَإِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَحۡدَهُ ٱشۡمَأَزَّتۡ قُلُوبُ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِۖ وَإِذَا ذُكِرَ ٱلَّذِينَ مِن دُونِهِۦٓ إِذَا هُمۡ يَسۡتَبۡشِرُونَ

Na Anapotajwa Mwenyezi Mungu Peke Yake zinachukia nyoyo za wasioamini Marejeo na Ufufuzi baada ya kufa, na wanapotajwa wale wasiokuwa Yeye miongoni masanamu, mizimu na wategemewa huwa wakifurahika kwa kuwa ushirikina unaafikiana na matamanio yao. info
التفاسير:

external-link copy
46 : 39

قُلِ ٱللَّهُمَّ فَاطِرَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ عَٰلِمَ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ أَنتَ تَحۡكُمُ بَيۡنَ عِبَادِكَ فِي مَا كَانُواْ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ

Sema, «Ewe Mwenyezi Mungu! Ewe Muumba mbingu na ardhi, Mwenye kuanzisha kuzitengeneza bila kuwa na mfano uliotangulia! Mjuzi wa siri na dhahiri! Wewe unatoa uamuzi baina ya waja wako Siku ya Kiyama katika yale ambayo walikuwa wakitafautiana juu yake ya maneno kuhusu wewe, ukubwa wako, utawala wako na kuhusu kukuamini wewe na kumuamini Mtume wako. Niongoze mimi kwenye haki ambayo kumetafautiana juu yake kwa amri yako. Hakika wewe unamuongoza unayemtaka kwenye njia iliyolingana sawa.» Hii ilikuwa ni miongoni mwa dua za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, nayo ina mafundisho kwa waja watake himaya kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na wamuombe kwa mjina Yake mazuri na sifa Zake tukufu. info
التفاسير:

external-link copy
47 : 39

وَلَوۡ أَنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا وَمِثۡلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفۡتَدَوۡاْ بِهِۦ مِن سُوٓءِ ٱلۡعَذَابِ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَبَدَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مَا لَمۡ يَكُونُواْ يَحۡتَسِبُونَ

Na lau hao wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu wangalikuwa nacho kila kilichoko kwenye ardhi miongoni mwa mali, vitu vya thamani na vingine mfano wake pamoja navyo kuongezea, wangalikitoa Siku ya Kiyama ili wajikomboe kwacho na adhabu mbaya. Na lau wangalikitoa na wakataka kujikomboa kwacho hakingalikubaliwa kutoka kwao na hakingaliwafalia kitu chochote kuwaepushia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na itawadhihirikia wao Siku hiyo amri ya Mwenyezi Mungu na adhabu Yake wasizokuwa wakizidhania duniani kuwa zitawashukia. info
التفاسير: