Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

Nomor Halaman:close

external-link copy
85 : 28

إِنَّ ٱلَّذِي فَرَضَ عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٖۚ قُل رَّبِّيٓ أَعۡلَمُ مَن جَآءَ بِٱلۡهُدَىٰ وَمَنۡ هُوَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ

Hakika Yule Aliyekuteremshia wewe, Qur’ani, ewe Mtume, na akakulazimisha wewe uifikishe na ushikamane nayo, ni Mwenye kukurudisha kule ulikotoka, nako ni Makkah. Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mola wangu Anamjua zaidi yule aliyeleta uongofu na yule ambaye ameenda nje ya haki waziwazi.» info
التفاسير:

external-link copy
86 : 28

وَمَا كُنتَ تَرۡجُوٓاْ أَن يُلۡقَىٰٓ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبُ إِلَّا رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرٗا لِّلۡكَٰفِرِينَ

Na hukuwa ukitarajia, ewe Mtume, kuteremkiwa na Qur’ani, lakini Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika na kutukuka, Alikurehemu Akakuteremshia. Basi mshukuru Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kwa neema Zake, na usiwe ni mwenye kuwasaidia watu wa ushirikina na upotevu. info
التفاسير:

external-link copy
87 : 28

وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بَعۡدَ إِذۡ أُنزِلَتۡ إِلَيۡكَۖ وَٱدۡعُ إِلَىٰ رَبِّكَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ

Na wasikuepushe wewe washirikina hawa na ufikishaji aya za Mola wako na hoja Zake baada ya kuwa Amekuteremshia kwako, na ufikishe ujumbe wa Mola wako, na usiwe ni miongoni mwa washirikina katika kitu chochote. info
التفاسير:

external-link copy
88 : 28

وَلَا تَدۡعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَۘ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ كُلُّ شَيۡءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجۡهَهُۥۚ لَهُ ٱلۡحُكۡمُ وَإِلَيۡهِ تُرۡجَعُونَ

Wala usiabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, muabudiwa mwingine. Hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kila kitu ni chenye kuangamia na kutoeka isipokuwa uso Wake. Uamuzi ni Wake. Na Kwake Yeye mutarudishwa baada ya kufa kwenu ili muhesabiwe na mulipwe. Katika aya hii kuna kuthibitisha sifa ya uso wa Mwenyezi Mungu, aliyetukuka, kama inavyonasibiana na ukamilifu Wake, ukubwa Wake na utukufu Wake. info
التفاسير: