Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Abdullah Muhammad dan Nasir Khamis

external-link copy
23 : 24

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَرۡمُونَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ٱلۡغَٰفِلَٰتِ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ لُعِنُواْ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ

Kwa kweli wale wanaowasingizia kitendo cha uzinifu wanawake wenye kujihifadhi, wasiofikiria machafu na walio Waumini ambao halijawapitia jambo hilo kwenye nyoyo zao, hao ni wenye kufukuzwa kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu , duniani na Akhera, na watapata adhabu kubwa kwenye moto wa Jahanamu. Kwenye aya hii kuna ushahidi juu ya ukafiri wa mwenye kumtukana au kumtuhumu mke yoyote kati ya wake za Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa jambo ovu lolote. info
التفاسير: