क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अली मुहसिन बरवानी

external-link copy
40 : 21

بَلۡ تَأۡتِيهِم بَغۡتَةٗ فَتَبۡهَتُهُمۡ فَلَا يَسۡتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمۡ يُنظَرُونَ

Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza kuurudisha, wala hawatapewa muhula! [40] info

[40] Kiyama hakiwajii kwa kukitarajia kutokea kwake, bali kitawazukia kwa ghafla tu kiwababaishe, wasiweze kukirudisha, wala wao hawatapewa muhula wa kutubia na kutafuta udhuru kwa waliyo kwisha yatenda..

التفاسير: