क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - सवाहिली अनुवाद - अली मुहसिन बरवानी

Al-Masad

external-link copy
1 : 111

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِي لَهَبٖ وَتَبَّ

Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia. info

Imeteketea mikono ya Abu Lahab iliyo kuwa ikiwaudhi Waislamu, na yeye mwenyewe amehiliki pia.

التفاسير:

external-link copy
2 : 111

مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُۥ وَمَا كَسَبَ

Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma. info

Hayatolindwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu mali yake aliyo kuwa nayo, wala cheo chake alicho kichuma.

التفاسير:

external-link copy
3 : 111

سَيَصۡلَىٰ نَارٗا ذَاتَ لَهَبٖ

Atauingia Moto wenye mwako. info

Ataingia katika Moto unao waka, aungue.

التفاسير:

external-link copy
4 : 111

وَٱمۡرَأَتُهُۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ

Na mkewe, mchukuzi wa kuni, info

Na ataingia pia kwenye Moto mkewe huyo aliye kuwa akibeba masengenyo baina ya watu, kama alivyo ingia yeye (mumewe).

التفاسير:

external-link copy
5 : 111

فِي جِيدِهَا حَبۡلٞ مِّن مَّسَدِۭ

Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa. info

Juu ya shingo yake itakuwa kamba ya mtende ya kumtesa.

التفاسير: