क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस

Al-Mutaffifin

external-link copy
1 : 83

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ

Adhabu kali ni ya wale wanaopunja vipimo vya vibaba na mezani. info
التفاسير:

external-link copy
2 : 83

ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ

Ambao wakinunua kwa watu cha kupimwa kwa vibaba au kwa mizani hujikamilishia wao wenyewe. info
التفاسير:

external-link copy
3 : 83

وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ

Na wakiwauzia watu kinachouzwa kwa vibaba au mizani wanapunguza vipimo. info
التفاسير:

external-link copy
4 : 83

أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ

Basi itakuwaje hali ya yule anayeiba na kupunja katika vipimo vyote hivyo, au yule anayeiba katika vipimo hivyo na huku awapunja watu vitu vyao? Hakika huyo yuwastahiki mateso zaidi kuliko wapunguzaji wa vipimo vya vibaba na mizani. Kwani hawaamini wale wapunjaji ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kuwafufua na kuwahesabu juu ya vitendo vyao. info
التفاسير: