क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस

पृष्ठ संख्या:close

external-link copy
36 : 33

وَمَا كَانَ لِمُؤۡمِنٖ وَلَا مُؤۡمِنَةٍ إِذَا قَضَى ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَمۡرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ ٱلۡخِيَرَةُ مِنۡ أَمۡرِهِمۡۗ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلٗا مُّبِينٗا

Na haipasi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke iwapo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wametoa uamuzi wawe wataenda kinyume nao, kwa kuchagua lile ambalo silo alilolihukumu kwao. Na anayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, amekuwa mbali na njia ya sawa umbali ulio wazi. info
التفاسير:

external-link copy
37 : 33

وَإِذۡ تَقُولُ لِلَّذِيٓ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَأَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِ أَمۡسِكۡ عَلَيۡكَ زَوۡجَكَ وَٱتَّقِ ٱللَّهَ وَتُخۡفِي فِي نَفۡسِكَ مَا ٱللَّهُ مُبۡدِيهِ وَتَخۡشَى ٱلنَّاسَ وَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخۡشَىٰهُۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيۡدٞ مِّنۡهَا وَطَرٗا زَوَّجۡنَٰكَهَا لِكَيۡ لَا يَكُونَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ حَرَجٞ فِيٓ أَزۡوَٰجِ أَدۡعِيَآئِهِمۡ إِذَا قَضَوۡاْ مِنۡهُنَّ وَطَرٗاۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولٗا

Na pindi unaposema, ewe Nabii, kumwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu Amemneemesha kwa Uislamu, naye ni Zayd bin Harithah ambaye Mtume , rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na wewe ukamneemesha kwa kumuacha huru, «Baki na mke wako, Zaynab binti Jahsh, na usimuache! na muogope Mwenyezi Mungu , ewe Zayd!» na huku unaficha, ewe Nabii, katika nafsi yako kile Alichokuletea wahyi nacho Mwenyezi Mungu cha Zayd kumuacha Zaynab na kuwa wewe utamuoa. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni Mwenye kudhihirisha ulichokificha, na unaogopa wasije wanafiki wakasema kwamba Muhammad amemuoa mtalaka wa mwanawe wa kubandika, na Mwenyezi Mungu Anastahiki zaidi umuogope. Basi Zayd alipomaliza haja yake kwa Zaynab na akamuacha kisha eda lake likamalizika, tulikuoza wewe, ili uwe ni kiigizo katika kubatilisha mila ya uharamishaji wa kuoa mke wa mwana wa kubandika baada ya kuachwa, wala haitakuwa kosa na dhambi kwa Wamini kuwaoa wake za wale watoto wao wa kubandika baada kuwaacha iwapo wamemaliza haja yao kwao. Na kwa hakika amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kufanyika, hakuna mwenye kuiwekea pingamizi wala kuizuia. Ada ya kujibandika mtoto ilikuwako zama za kijinga (kabla ya Uislamu) kisha ikabatilishwa kwa neno lake Mwenyezi Mungu, «Waiteni wao kwa kuwanasibisha na baba zao..». info
التفاسير:

external-link copy
38 : 33

مَّا كَانَ عَلَى ٱلنَّبِيِّ مِنۡ حَرَجٖ فِيمَا فَرَضَ ٱللَّهُ لَهُۥۖ سُنَّةَ ٱللَّهِ فِي ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلُۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ قَدَرٗا مَّقۡدُورًا

Haikuwa ni dhambi kwa Nabii Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, katika kile Alichomhalalishia Mwenyezi Mungu cha kumuoa mke wa mwanawe wa kujibandika baada ya kumuacha, kama vile alivyowahalalishia hilo Manabii kabla yake yeye, ni mwenendo uliowekwa na Mwenyezi Mungu kwa wale waliopita kabla. Na kwa kweli, amri ya Mwenyezi Mungu ni mpango uliokadiriwa , hauna budi kutokea. info
التفاسير:

external-link copy
39 : 33

ٱلَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَٰلَٰتِ ٱللَّهِ وَيَخۡشَوۡنَهُۥ وَلَا يَخۡشَوۡنَ أَحَدًا إِلَّا ٱللَّهَۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا

Kisha Mwenyezi Mungu, Aliyetakasika, Aliwataja Manabii waliopita na Akawasifu kwamba wao ni wale wanaozifikisha jumbe za Mwenyezi Mungu kwa watu, na wanamuogopa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na hawamuogopi yoyote asiyekuwa Yeye. Na inatosha kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwahesabu waja Wake kwa matendo yao yote na ni Mwenye kuyaona. info
التفاسير:

external-link copy
40 : 33

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٖ مِّن رِّجَالِكُمۡ وَلَٰكِن رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا

Hakuwa Muhammad ni baba wa yoyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Manabii, hakuna unabii baada yake mpaka Siku ya Kiyama. Na Mwenyezi Mungu kwa kila jambo miongoni mwa matendo yenu ni mjuzi, hakuna chenye kufichamana Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
41 : 33

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ ذِكۡرٗا كَثِيرٗا

Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo, mtajeni Mwenyezi Mungu kwa nyoyo zenu, ndimi zenu na viungo vyenu utajo mwingi sana. info
التفاسير:

external-link copy
42 : 33

وَسَبِّحُوهُ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلًا

Na zishughulisheni nyakati zenu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, asubuhi na jioni, baada ya Swala za faradhi na nyakati za matukio maalumu na sababu, kwani huko kumtaja Mwenyezi Mungu ni ibada iliowekwa na Sheria, inapelekea kwenye mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kujizuia na madhambi, na inasaidia kila kheri. info
التفاسير:

external-link copy
43 : 33

هُوَ ٱلَّذِي يُصَلِّي عَلَيۡكُمۡ وَمَلَٰٓئِكَتُهُۥ لِيُخۡرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَكَانَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَحِيمٗا

Yeye Ndiye Anayewarehemu na kuwasifu, na Malaika Wake wanawaombea dua, ili awatoe kutoka kwenye giza la ujinga na upotevu kuwaelekeza kwenye nuru ya Uislamu.Na ni Mwenye kuwarehemu Waumini duniani na Akhera, hawaadhibu wao maadamu wao waendelea kumtii na kumtakasa. info
التفاسير: