કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

Qamar

external-link copy
1 : 54

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ

Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! info

Kiyama kimekaribia na mwezi utapasuka hapana hivi wala hivi.

التفاسير:

external-link copy
2 : 54

وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ

Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. info

Na makafiri wakiona Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni uchawi wa daima unaendelea!

التفاسير:

external-link copy
3 : 54

وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ

Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. info

Na wamewakanusha Mitume na wakafuata yaliyo zainishwa na matamanio yao. Na kila jambo huishia mwisho wake linapo tulia na kuthibiti.

التفاسير:

external-link copy
4 : 54

وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ

Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio. info

Na ninaapa kuwa zimewajia makafiri khabari za mataifa yaliyo tangulia zenye ukweli wa uumbaji ambazo zina mikemeo ya kutosha.

التفاسير:

external-link copy
5 : 54

حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ

Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu! info

Haya yaliyo wajia ni hikima kubwa na lengo la kufikia mbali. Lakini maonyo yataleta faida gani kwa wanao zipinga hikima hizo?

التفاسير:

external-link copy
6 : 54

فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَيۡءٖ نُّكُرٍ

Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; . info

Ewe Muhammad! Waachilie mbali hawa makafiri, nawe ngojea siku atapoita mwitaji wa Mwenyezi Mungu kuitia jambo ambalo nafsi inalichukia mno!

التفاسير: