કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અલી મોહસીન અલ્ બર્વાની

external-link copy
118 : 5

إِن تُعَذِّبۡهُمۡ فَإِنَّهُمۡ عِبَادُكَۖ وَإِن تَغۡفِرۡ لَهُمۡ فَإِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Ukiwaadhibu basi hao ni waja wako. Na ukiwasamehe basi Wewe ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikima. info

Ukiwaadhibu kwa waliyo yatenda basi hao ni waja wako, unawafanya upendavyo. Na ukiwasamehe, basi hakika Wewe peke yako ndiye Mtenda nguvu usiye shindwa, Mwenye hikima yenye kufikilia kila linalo toka kwako.

التفاسير: