[84] Na kama wapo kati yenu mfano wa hawa wanaafiki basi wapuuzilie mbali. Na wewe pigana kwa ajili ya Neno la Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Haki. Wewe huna jukumu ila la nafsi yako tu. Kisha waite Waumini wende vitani, na wahimize. Huenda Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwako na kwao akazuia hayo mashambulio ya makafiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukuungeni mkono, na ni Mwenye kukunusuruni. Na Yeye ana nguvu kuliko wote, na mkali kuliko wote katika kuwaadhibu makafiri.