[58] Watu hawa hawazingatii yaliyo wapata kaumu zilizo kwisha tangulia. Iliangamizwa miji ya walio ghurika na neema za Mwenyezi Mungu, na kisha wakazikanusha na wakamkanusha Mwenyezi Mungu. Na haya majumba yao yamekuwa matupu, magofu, hayafai kukaliwa ila nadra tu kwa wapita njia. Na yamebaki hayana mwenye kuyamiliki baada yao ila Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu na ukarimu.