કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અબ્દુલ્લાહ મુહમ્મદ અને નાસિર ખમીસ

પેજ નંબર:close

external-link copy
48 : 9

لَقَدِ ٱبۡتَغَوُاْ ٱلۡفِتۡنَةَ مِن قَبۡلُ وَقَلَّبُواْ لَكَ ٱلۡأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَظَهَرَ أَمۡرُ ٱللَّهِ وَهُمۡ كَٰرِهُونَ

Walipendelea wanafiki kuwafitini Waumini na Dini yao na kuwazuia wasiiifuate njia ya Mwenyezi Mungu kabla ya vita vya Tabūk, na mambo yao yakafunuka wakajulikana. Na walikuchafulia mambo, ewe Nabii, katika kuyavunja uliyokuja nayo, kama walivyofanya siku ya vita vya Uḥud na siku ya vita vya Khandaq. Na walikufanyia vitimbi mpaka usaidizi ukaja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Akawatia nguvu askari Wake na Akaipa ushindi dini Yake, pamoja na kuwa wao wanaichukia. info
التفاسير:

external-link copy
49 : 9

وَمِنۡهُم مَّن يَقُولُ ٱئۡذَن لِّي وَلَا تَفۡتِنِّيٓۚ أَلَا فِي ٱلۡفِتۡنَةِ سَقَطُواْۗ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ

Miongoni mwa wanafiki hawa, kuna wale wanaoomba ruhusa ya kuketi wasiende kwenye jihadi na wanasema, «Usiniingize kwenye mtihani utakaonifikia, katika hali ya kutoka, wa fitina ya kuvutiwa na wanawake.» Hakika wanafiki hawa wameanguka kwenye fitina kubwa ya unafiki. Na kwa hakika, Moto wa jahanamu ni wenye kuwazunguka wanaomkanusha Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho; hakuna atakayeponyoka. info
التفاسير:

external-link copy
50 : 9

إِن تُصِبۡكَ حَسَنَةٞ تَسُؤۡهُمۡۖ وَإِن تُصِبۡكَ مُصِيبَةٞ يَقُولُواْ قَدۡ أَخَذۡنَآ أَمۡرَنَا مِن قَبۡلُ وَيَتَوَلَّواْ وَّهُمۡ فَرِحُونَ

Ewe Nbii! Unapofikiwa na furaha na ngawira, wanafiki wanasikitika, na unapopatwa na kero la kushindwa au matatizo, wanasema,»Sisi ni wenye busara na uhodari wa kupanga, tulijipangia kwa maslahi yetu kubakia nyuma na kutomfuata Muhammad.» Na hapo wanaondoka hali ya kuwa na furaha kwa waliyoyafanya na kwa mabaya yaliyokufika. info
التفاسير:

external-link copy
51 : 9

قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوۡلَىٰنَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Sema, ewe Nabii, uwaambie hao wanaovunja moyo kwa kujitoa, kwa kuwakemea na kuwaumbua, «Hakuna litakalotupata isipokuwa lile Alilolipitisha Mwenyezi Mungu juu yetu na Aliloliandika katika al-Lawḥ al-Maḥfūẓ (Ubao Uliohifadhiwa). Yeye Ndiye Mwenye kutupa ushindi juu ya maadui wetu.» Na kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na wajitegemeze wale wanaoumuamini. info
التفاسير:

external-link copy
52 : 9

قُلۡ هَلۡ تَرَبَّصُونَ بِنَآ إِلَّآ إِحۡدَى ٱلۡحُسۡنَيَيۡنِۖ وَنَحۡنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمۡ أَن يُصِيبَكُمُ ٱللَّهُ بِعَذَابٖ مِّنۡ عِندِهِۦٓ أَوۡ بِأَيۡدِينَاۖ فَتَرَبَّصُوٓاْ إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ

Waambie, ewe Nabii, «Kwani kuna mnachokitazamia kwetu isipokuwa tufe mashahidi au tuwashinde? Na sisi tunatazamia kwenu kwamba Mwenyezi Mungu Atawapatia mateso ya haraka yanayotoka Kwake yawaangamize, au yanayotokana na mikono yetu tuwaue. Basi ngojeeni, na sisi tunalingojea, pamoja na nyinyi, lile ambalo Mwenyezi Mungu ni Mwenye kulifanya kwa kila kundi kati yetu na nyinyi.» info
التفاسير:

external-link copy
53 : 9

قُلۡ أَنفِقُواْ طَوۡعًا أَوۡ كَرۡهٗا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمۡ إِنَّكُمۡ كُنتُمۡ قَوۡمٗا فَٰسِقِينَ

Sema, ewe Nabii, kuwaambia wanafiki, «Toeni mali zenu vile mtakavyo na namna mtakavyo, kwa hiari yenu au kwa kulazimishwa, Mwenyezi Mungu hatavikubali kutoka kwenu mnavyovitoa, kwa kuwa nyinyi ni watu mliotoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu na utiifu Kwake. info
التفاسير:

external-link copy
54 : 9

وَمَا مَنَعَهُمۡ أَن تُقۡبَلَ مِنۡهُمۡ نَفَقَٰتُهُمۡ إِلَّآ أَنَّهُمۡ كَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأۡتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمۡ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمۡ كَٰرِهُونَ

Na sababu ya kutokubaliwa wanavyovitoa ni kwamba wao wameficha ukanushaji wao Mwenyezi Mungu, Aliyeshinda na kutukuka, na ukataaji wao ukweli wa Mtume Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na kwamba wao hawaendi kuswali isipokuwa huku wanaona uzito, na kwamba hawatoi mali yao isipokuwa huku wao ni wenye kuchukia hilo. Wao hawana matarajio ya kupata malipo ya faradhi hizi wala hawaogopi mateso kwa kuziacha kwa ukafiri wao walionao. info
التفاسير: