કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અબ્દુલ્લાહ મુહમ્મદ અને નાસિર ખમીસ

પેજ નંબર:close

external-link copy
18 : 23

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءَۢ بِقَدَرٖ فَأَسۡكَنَّٰهُ فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابِۭ بِهِۦ لَقَٰدِرُونَ

Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kadiri ya mahitaji ya viumbe, na tumeifanya ardhi kuwa ni mahali pa kutulia haya maji, na sisi niwaweza wa kuyaondoa maji haya yaliyotulia. Katika haya pana kitisho na onyo kwa wenye udhalimu. info
التفاسير:

external-link copy
19 : 23

فَأَنشَأۡنَا لَكُم بِهِۦ جَنَّٰتٖ مِّن نَّخِيلٖ وَأَعۡنَٰبٖ لَّكُمۡ فِيهَا فَوَٰكِهُ كَثِيرَةٞ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Tukawafanyia kwa maji haya mashamba ya mitende na mizabibu, mukawa nayo nyinyi kutokana na mashamba hayo matunda ya aina nyingi na sampuli mbalimbali, na katika hayo munakula. info
التفاسير:

external-link copy
20 : 23

وَشَجَرَةٗ تَخۡرُجُ مِن طُورِ سَيۡنَآءَ تَنۢبُتُ بِٱلدُّهۡنِ وَصِبۡغٖ لِّلۡأٓكِلِينَ

Na tukawatolea nyinyi kwa maji hayo mizaituni ambayo inatoka kandokando ya jabali la Tūr Ṣīnā’ ambao unakamuliwa mafuta ya kujipaka na kutumia kwa chakula. info
التفاسير:

external-link copy
21 : 23

وَإِنَّ لَكُمۡ فِي ٱلۡأَنۡعَٰمِ لَعِبۡرَةٗۖ نُّسۡقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهَا وَلَكُمۡ فِيهَا مَنَٰفِعُ كَثِيرَةٞ وَمِنۡهَا تَأۡكُلُونَ

Na nyinyi, enyi watu, muna mazingatio katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo ya kulizingatia namna ya kuumbwa kwao. Tunawanywesha maziwa yanayotoka matumboni mwao. Na munayo nyinyi kutokana nao manufaa mengine mengi kama sufi na ngozi na mfano wa hivyo, na miongoni mwao mnakula. info
التفاسير:

external-link copy
22 : 23

وَعَلَيۡهَا وَعَلَى ٱلۡفُلۡكِ تُحۡمَلُونَ

Na juu ya ngamia na majahazi, katika nchi kavu na baharini munabebwa. info
التفاسير:

external-link copy
23 : 23

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Kwa hakika, tulimtumiliza Nūḥ kwa watu wake kuwalingania kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, (alipokwenda) akawaambia, «Muabuduni Mwenyezi Mungu peke Yake, nyinyi hamuna muabudiwa yoyote isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, basi mtakasieni ibada. Kwani nyinyi hamuiogopi adhabu yake?» info
التفاسير:

external-link copy
24 : 23

فَقَالَ ٱلۡمَلَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ مَا هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيۡكُمۡ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَنزَلَ مَلَٰٓئِكَةٗ مَّا سَمِعۡنَا بِهَٰذَا فِيٓ ءَابَآئِنَا ٱلۡأَوَّلِينَ

Basi wale waheshimiwa wa watu wake walimkanusha na wakasema kuwaambia watu wa kawaida wao, «Yeye ni mwanadamu kama nyinyi, hana ubora wowote wa kutafautiana na nyinyi, na hataki kwa maneno yake isipokuwa uongozi na utukufu juu yenu, na lau Mwenyezi Mungu Alitaka kutuletea mtume, Angalimtuma Malaika kwetu, hatujasikia mfano wa hili kwa watu waliotutangulia miongoni mwa mababa na mababu. Na huyu Nūh info
التفاسير:

external-link copy
25 : 23

إِنۡ هُوَ إِلَّا رَجُلُۢ بِهِۦ جِنَّةٞ فَتَرَبَّصُواْ بِهِۦ حَتَّىٰ حِينٖ

hakuwa isipokuwa ni mwanamume aliyeshikwa na wazimu, basi ngojeeni mpaka atakapopata fahamu auache ulinganizi wake au afe mupumzike na yeye.» info
التفاسير:

external-link copy
26 : 23

قَالَ رَبِّ ٱنصُرۡنِي بِمَا كَذَّبُونِ

Nūḥ akasema, «Mola wangu! Niokoe na watu wangu kwa sababu ya kunikanusha mimi kwa yale niliyowafikishia ya ujumbe wako.» info
التفاسير:

external-link copy
27 : 23

فَأَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡهِ أَنِ ٱصۡنَعِ ٱلۡفُلۡكَ بِأَعۡيُنِنَا وَوَحۡيِنَا فَإِذَا جَآءَ أَمۡرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ فَٱسۡلُكۡ فِيهَا مِن كُلّٖ زَوۡجَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِ وَأَهۡلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيۡهِ ٱلۡقَوۡلُ مِنۡهُمۡۖ وَلَا تُخَٰطِبۡنِي فِي ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓاْ إِنَّهُم مُّغۡرَقُونَ

Hapo tukamletea wahyi na kumwambia, «Tengeneza jahazi chini ya uangalizi wetu na amri yetu kwako na usaidizi wetu, na wewe uko kwenye utunzi wetu na hifadhi yetu. Basi amri yetu itakapokuja ya kuwaadhibu watu wako kwa kuwazamisha, na mafuriko yakaanza, na maji yakatembuka kwa nguvu kwenye tanuri, napo ni mahali pa kuchomea mikate, ikiwa ni alama ya kuja kwa adhabu, hapo basi watie ndani ya jahazi, kati ya kila kilicho hai, kiume na kike, ili kizazi kisalie. Na uwatie watu wako pia, isipokuwa yule aliyestahili kuadhibiwa kwa ukafiri wake, kama mke wako na mwano wa kiume, na usiniombe kuokolewa watu wako waliodhulumu, kwani wao hapana budi ni wenye kuzamishwa. Na katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya jicho kwa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, kama inavyonasibiana na Yeye, Aliyetukuka, bila kufananisha wala kulifanya liko namna gani. info
التفاسير: