કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષામાં અનુવાદ - અબ્દુલ્લાહ મુહમ્મદ અને નાસિર ખમીસ

પેજ નંબર:close

external-link copy
257 : 2

ٱللَّهُ وَلِيُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُخۡرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَوۡلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّٰغُوتُ يُخۡرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَٰتِۗ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Mwenyezi Mungu Anawasimamia Waumini kwa kuwanusuru, kuwaafikia na kuwahifadhi, Anawatoa kutoka kwenye magiza ya ukafiri kuwapeleka kwenye nuru ya Imani. Na wale waliokufuru, wanusuru wao na wasaidizi wao ni wale wafananishwao na Mwenyezi Mungu na masanamu wanaowaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu. Hao wanawatoa wao kutoka kwenye nuru ya Imani kuwapeleka kwenye magiza ya ukafiri. Wao ndio watu wa Motoni wenye kutindikia humo, wenye kusalia humo milele na si wenye kutoka humo. info
التفاسير:

external-link copy
258 : 2

أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِي حَآجَّ إِبۡرَٰهِـۧمَ فِي رَبِّهِۦٓ أَنۡ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ رَبِّيَ ٱلَّذِي يُحۡيِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۠ أُحۡيِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٰهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِي بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِهَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِي كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Je umewahi kuona, ewe Mtume, hali ya kustaajabisha zaidi kuliko ile ya yule aliyemjadili Ibrāhīm, amani imshukie, juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na juu ya uola Wake, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimpa ufalme, alipofanya ujeuri na kumuuliza Ibrāhīm, «Ni nani Mola wako?» Alisema, amani imshukie, «Mola wangu ni Ambaye Anavipa viumbe uhai vikahuika na Anaviondolea uhai vikafa. Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa kuhuisha na kufisha.» Akasema, «Mimi nahuisha na kufisha.» Yaani: namuua nimtakaye kumuua, na namuachilia nimtakaye kumuachilia. Ibrāhīm akasema kumwambia, «Mwenyezi Mungu ninayemuabudu Analitoa jua upande wa mashariki. Je unaweza wewe kugeuza mwenendo huu wa kimungu, ulifanye litokeze upande wa magharibi?» Akapigwa na mshangao huyu kafiri na ikakatika hoja yake. Hali yake ni ile ya madhalimu, Mwenyezi Mungu Hawaongozi kwenye haki na usawa. info
التفاسير:

external-link copy
259 : 2

أَوۡ كَٱلَّذِي مَرَّ عَلَىٰ قَرۡيَةٖ وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحۡيِۦ هَٰذِهِ ٱللَّهُ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۖ فَأَمَاتَهُ ٱللَّهُ مِاْئَةَ عَامٖ ثُمَّ بَعَثَهُۥۖ قَالَ كَمۡ لَبِثۡتَۖ قَالَ لَبِثۡتُ يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٖۖ قَالَ بَل لَّبِثۡتَ مِاْئَةَ عَامٖ فَٱنظُرۡ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمۡ يَتَسَنَّهۡۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجۡعَلَكَ ءَايَةٗ لِّلنَّاسِۖ وَٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡعِظَامِ كَيۡفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكۡسُوهَا لَحۡمٗاۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥ قَالَ أَعۡلَمُ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Au je uliona, ewe Mtume, mfano wa yule aliyepita kwenye kijiji ambacho nyumba zake zilikuwa zimevunjika na kuangukia misingi yake na akasema, «Vipi Mwenyezi Mungu Atakihuisha kijiji hiki baada ya kuwa kimekufa?» Mwenyezi Mungu Akamfisha miaka mia moja kisha Akamrudishia roho yake na Akamwambia, «Ni kwa muda gani ulikuwa umekufa?» Akasema, «Nilikuwa nimekufa kwa muda wa siku moja au sehemu ya siku.» Akampa habari kuwa alikuwa amekufa kwa muda wa miaka mia. Na Akamuamrisha akiangalie chakula chake na kinywaji chake vipi Mwenyezi Mungu Amevihifadhi visiharibike muda huu mrefu. Na Akamuamrisha amtazame punda wake aone vipi Mwenyezi Mungu Alimuhuisha baada ya kuwa mifupa iliyotapakaa. Na Akamwambia, «Na ili tukufanye wewe ni dalili kwa watu.» Yaani: dalili iliyo wazi ya uweza wa Mwenyezi Mungu kufufua baada ya kufa. Na akamuamrisha aitazame mifupa aone vipi Mwenyezi Mungu Anavyoiinua baadhi yake juu ya mingine na kuiunganisha baadhi yake na mingine na kuivisha nyama baada ya kushikana na kisha kuirudishia uhai.Yalipomfunukia hayo waziwazi alikubali ukubwa wa Mwenyezi Mungu na kuwa Yeye ni Muweza wa kila kitu. Na akawa ni dalili kwa watu. info
التفاسير: